Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoro Bi. Ziada Sellah akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo wezeshi ya kujadili namna ya uboreshaji wa huduma za ukunga nchini,jijini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo wezeshi wakifuatilia uwasilishaji wa mada zilizotolewa kwenyemkutano huo ambao uliwashirikisha Wizara ya Afya, TAMISEMI, Wakufunzi wa Vyuo pamoja na Chama cha Wakunga Tanzania(TAMA)
Wadau walioshiriki mafunzo hayo ambayo yalijadili namna ya kutoa huduma za uuguzi na ukunga zinazofuata weledi na huduma kwa mteja katika kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi na watoto wachanga kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma
Picha ya pamoja ya washiriki kutoka sehemu mbalimbali
………………………………………………………………………
Na WAJMW-Dodoma
Wadau wa Uuguzi na Ukunga wamekutana na kupanga mikakati ya kupunguza vifo
vitokananvyo na uzazi na watoto wachanga kwa kuhakikisha huduma zinakuwa bora
ikiwa ni Pamoja na kushirikisha walimu wa vyuo mbalimbali vinavyozalisha
wanafunzi wa taaluma hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa huduma na Ukunga na Uuguzi kutoka
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ziada Sellah
wakati akifungua semina fupi kwa niaba ya Mganga mkuu wa Serikali ambapo
semina hiyo iliwashirikisha Wizara ya afya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI,wakufunzi wa
vyuo na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kwenye hospitali ya Benjamin
Mkapa jijini hapa.
“Tumeangalia kwa upana wake na kuweka mikakati mbalimbali ya jinsi huduma
zinazotolewa na wakunga kwa wajawazito ikiwa ni Pamoja na kuwapa mazingira
wezeshi, huduma nzuri kwa wateja lakini pia tumewashirikisha walimu wa vyuo vya
ukunga ili wafundishe somo la huduma kwa mteja ili isijekua ni kitu kipya kwa
wanafunzi wanapoingia kazini”. Amesema Bi. Ziada.
Bi. Ziada amesema Wizara kupitia kurugenzi ya Uuguzi na ukunga itahakikisha
wakunga wanapata mafunzo wakiwa maeneo yao ya kazi kupitia kwa wauguzi
wakuu wa Wilaya na Mikoa pamoja na wauguzi viongozi ili kuweza kuboresha
ukunga lengo likiwa ni kupunguza vifo vitokavyo na uzazi.
“Tumeangalia kwa upana kuanzia huduma zinapoanza kutolewa upande wa huduma
ya Uzazi,Mama na Mtoto pale mama anapoanza kliniki na kuelekeza jinsi gani ya
kutoa huduma ikiwemo vidokezo hatarishi kwa mama mjamzito pamoja na kutoa
rufaa nmapema endapo kesi hawatoiweza,hivyo tutawajengea uwezo wakunga
kwani asilimia 90 ya akina mama wote wanaojifungua wanahudumiwa na wakunga”.
Alisisitiza Bi. Ziada.
Naye Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania Chama cha Wakunga nchini (TAMA)
Bi. Fedy Mwanga amesema chama kimejidhatiti kutoa elimu kwa wauguzi na
wakunga nchini kuhusiana na huduma bora za uzazi kwa mama mjamzito kabla na
baada ya kujifungua lengo likiwa ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Amesema chama hicho kinaandaa makongamano kwa ajili ya wakunga nchini ili
waweze kupata elimu na kukumbushwa maadili katika utoaji wa huduma pale mama
mjamzito anapofika katika sehemu ya kutolea huduma za afya.
“Leo tumeita wadau mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza shughuli zetu za utetezi wa
kuimarisha shughuli za ukunga Tanzania kwa kujua kabisa vifo vitokanavyo na uzazi
nchini bado viko juu na vinazuilika, kwa kutambua umuhimu wa huduma za ukunga
katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi tunakutana ili kukumbushana wajibu
wetu katika kupunguza vifo hivyo”.Amesema Bi. Fedy.
Bi. Fedy amesema mkunga akiwa na stadi zinazostahili na akisimamiwa vizuri na
kufanya kazi katika mazingira wezeshi anaweza kumuhudumia mama na kupunguza
vifo kwa asilimia 87 hivyo chama cha wakunga nchini kina wajibu wa kufanya vikao
na wadau ili kuweza kujadili namna wanavyoweza kufanikisha mazingira wezeshi
kwa wakunga nchini.
Wakati huo huo Msimamizi wa huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka OR-TAMISEMI
Dinna Atinda amesema wataendelea kuboresha na kusimamia huduma za uuguzi na
ukunga kwenye halmashauri zote nchini ili watoa huduma ngazi zote wanapata
mafunzo na usimamizi mzuri ili kuendelea kutoa huduma nzuri na kwa uweledi kwa
wananchi na kuweza kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi.
Katika kukabiliana na changamoto za watumishi amesema serikali inaendelea kutoa
ajira kila mwaka kwa watumishi wenye sifa na weledi ili kuweza kupunguza vifo
vitokananvyo na uzazi na watoto wachanga.