Mjumbe Kamati Kuu CCM Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Singida ,Munde Tambwe,akizungumza na wanachama wa CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Manyoni Mashariki.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka akimnadi mgombe wa jimbo hilo Dkt.Pius Chaya wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Manyoni Mashariki.
Mbunge Mteule Viti Maalum Mkoa wa Singida Mhe.Martha Gwau ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Manyoni Mashariki.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Manyoni ,Jumanne Makhanda,akiongea kwenye Mkutano wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Manyoni Mashariki.
Mjumbe Kamati Kuu CCM Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Singida ,Munde Tambwe,akimnadi mgombea wa jimbo la Manyoni Mashariki Dk.Pius Chaya kwa wananchi na wanachama wa CCM waliohudhuria Kampeni kampeni za uchaguzi katika jimbo la Manyoni Mashariki.
Mgombea wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dk.Pius Chaya akiomba kura kwa wananchi na wanachama wa CCM wakati akizindua kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo.
Mjumbe Kamati Kuu CCM Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Singida ,Munde Tambwe,akimnadi mgombea wa udiwani Kata ya Manyoni Mjini ,Simon Mapunda wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa jimbo la Manyoni Mashariki.
Mgombea wa udiwani Kata ya Manyoni Mjini ,Simon Mapunda akiomba kura kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa jimbo la Manyoni Mashariki.
Baadhi ya wafuasi wa CCM wakicheza na kufurahi na Mgombea wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dk.Pius Chaya wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo.
Wanachama wa CHADEMA wakionyesha Bendera na T-shirt za chama hicho mara baada ya kuhamia CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo.
Wanachama wa CCM waliohudhuria uzinduzi wa kampeni za Mgombea wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dk.Pius Chaya wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo.
…………………………………………………………………………………
Na Alex Sonna, Manyoni
Mgombea ubunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dkt.Pius Chaya Ametaja vipaumbele atakavyovishughulikia katika kipindi chake iwapo akipata ridhaa kutoka kwa wananchi wa jimbo hilo kuwa ni pamoja na Afya, maji, Elimu, kilimo, michezo na ajira kwa vijana.
Dkt. Chaya amebainisha hayo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo wilayani Manyoni mkoani Singida.
Aidha Dkt.Chaya ameeleza kuwa utekelezaji wa vipaumbele hivyo utasaidia kuondoa changamoto kadhaa zilizopo katika jimbo hilo jimbo hilo.
Kwa upande wa Afya Dkt. Chaya amesisitiza kuwa katika kipindi chake atahakikisha anapigania upatikanaji wa hospitali ya wilaya ili kurahisisha huduma za matibabu kwa wananchi hususan kwa akina wajawazito na watoto.
“ Ntahakikisha wakina mama wajawazito wanaosubiri kujifungua wanakuwa na jengo la kisasa badala ya jengo waanalotumia sasa ambapo halina hadhi ya kuwaweka akina mama hao”, ameeleza Dkt. Chaya.
“Sasa hivi akina mama wajawazito wanaotoka vijijini na kusubiria kujifungua wanakaa jengo la tumbaku ,hii siyo sawa nitapigania upatikanajo wa jengo la kisasa kwa ajili ya akina mama hawa.” Amebainisha Dkt. Chaya.
Dkt. Chaya ameongeza kuwa atahakikisha tatizo la maji katika jimbo hilo litabaki historia, kwa katika sekta ya Elimu kuna baadhi ya kata hazina shule za sekondari lakini pia zipo shule za msingi ambazo hazijasajiliwa.
“Nitaweka vipaumbele kwenye ujenzi wa hosteli kwa ajili ya kuwqlibda watoto wa kike lakini pia nitashughulikia upatikanaji wa madawati mashuleni,” ameeleza Dkt. Chaya