Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Usagara wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza leo Jumanne Septemba 8,2020 wakati akiwa njiani kwenda mkoani Geita kwa ajili ya kuendelea na mikutano ya Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020 nchini kote.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-MISUNGWI)
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwawasikiliza wananchi wa Usagara wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza leo Jumanne Septemba 8,2020 wakati wakati alipokuwa akizungumza nao akiwa njiani kwenda mkoani Geita kwa ajili ya kuendelea na mikutano ya Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020 nchini kote.
Mbunge mteule wa jimbo la Misungwi Bw. Alexander Mnyeti akimuombea kura Mgombea Urais kupitia CCM Rais Dk John Pombe Magufuli katika mji wa Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Picha mbalimbali zikionesha wananchi wakimshangilia na kumsikiliza Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akizungumza nao akiwa njiani kwenda mkoani Geita.