Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Wananchi waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza.
(PICHA IKULU NA JOHN BUKUKU-MWANZA)
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Buchosa Bw. Eric Shigongo kwa Wananchi waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Alexander Mnyeti Mbunge mteule wa jimbo la Misungwi kwa Wananchi waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiondoka kwenye uwanja wa CCM Kirumba mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa CCM Kirumba mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza
Baadhi ya wagombea ubunge wa mkoa wa Mwanza wakicheza muziki wa msanii Zuchu mara baada ya mkutano huo kumalizika.
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia Wananchi waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba bara baada ya kumaliza khutubia Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Dk Ali Bashiru Kakurwa.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza kumsikiliza mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Baadhi ya madiwani na viongozi mbalimbali waliojitokeza kwenye mkutano huo wakipiga pushup mbele ya Rais Dk John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Wananchi waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria Mkutano wa Kampeni za Urais za Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo tarehe 7 Septemba 2020
……………………………………………….
Mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk John Pombe Magufuli amesema uamuzi wa kujenga barabara ya Kisesa kwa gharama ya Sh Bil 20.1 ulikuwa ni wa kimkakati ili kuondoa msongamani katikati ya jiji la Mwanza.
Kwa sababu Mwanza tunataka kuifanya kuwa kituo kikuu cha biashara katika nchi za Maziwa makuu ni lazima kujenga miundombinu yote itakayowezesha uneo hili kuwa na fursa nyingi za biashara na uwekezaji.
Rais Magufuli amesema hayo wakati akiwahutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
Ameongeza kuwa pamoja na hayo pia umefanyika ukarabati wa meli tano katika Ziwa Victoria na kutengeneza meli moja mpya kwa gharama ya Sh Bil 152 pamoja na vivuko viwili kwa Bil 2.7.
Ameongeza kuwa kwa sasa kinajengwa kivuko kingine kimoja kikubwa kwa gharama ya Sh Bil 4.2, ndani ya miaka mitano jijini Mwanza imejengwa barabara ya Airpory, Nyakato – Veta hadi Buswelo, Barabara ya Makongoro hadi Mwaloni, Isamilo hadi Mji Mwema, Pasiasi hadi Buzurugwa na daraja la Furahisha eneo ambao wananchi walikuwa wakigongwa na magari mara kwa mara bila kusahau Soko la Nyegezi.
Katika mkutano huo pia amezungumzia pia upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ambao umekuwa na uwezo wa kupokea ndege za kimataifa na kusafirisha minofu ya samaki kwenda Ulaya.
“Tangu safari ya kwanza ilipoanza Aprili mwaka huu tumefanikiwa kusafirisha nje ya nchi tani 109,000 ikiwa ni baada ya kuutanua uwanja huo kutoka kilomita 2.8 hadi kilomita 3.5. Tumeweka taa, eneo la maegesho ya ndege na eneo la kuhifadhia minofu ya samaki,” amesema Dk. Magufuli.
Aidha, alitaja suala la ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) Mwanza hadi Isaka kilomita 250, baadaye itaunganisha hadi Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa kwa ahadi aliyoitoa kwa wanamwanza mwaka 2015 anahitajika kufanya mambo makubwa mawili, kwanza kuimarisha miundombinu ya usafirishaji na huduma za jamii ikiwemo afya, elimu, maji na umeme. Kwa sababu unapotaka kujenga taifa lolote mambo haya ni ya msingi katika kukuza uchumi wa nchi, nashukuru tulifanya kazi kwa pamoja,” alibainisha.
Huu ni ujumbe kwa wanaojitokeza kuja kuomba kura, wataisoma namba. Kilichonifurahisha zaidi wananchi waliojaa hapa si wana CCM pekee ni wa vyama vyote kwa sababu wanaamini katika maendeleo, ahsanteni wana Mwanza ahsanteni Watanzania,” amesema Dk. Magufuli.
“Mimi Mwanza nina asili nayo nilisoma hapa miaka ya 1978 nilikuwa nikitembea kwa mguu umbali mrefu kwenda shuleni na kurudi nyumbani, wakati nikifanya kazi nilipanga kwa Mzee Gilya nikaishi Kitangiri kwa Mzee Kubanga baadaye nikajenga eneo la Selemani Nassoro,” amesema.