***************************************
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limepokea kwa huzuni na mshtuko mkubwa taarifa za vifo vya wadau nguli wa michezo ya Ngumi za kulipwa pamoja na Netiboli Tanzania, Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania
(TPBO), Yassin Abdallah almaarufu kama Ustadh pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa Netiboli Tanzania (CHANETA) MAMA Anna Faith Kibira.
Kaimu Mtendaji Mkuu Bi. Neema Msitha kwa niaba ya BMT ametoa pole kwa familia za marehemu, wanafamilia wa michezo,ndugu jamaa na marafiki.
“vifo vya nguli hawa wa michezo, vimenishtua sana na kwa niaba ya Baraza natoa pole kwa wafiwa nawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu kwao kuwapoteza wapendwa wao,hakika tutawakumbuka kwa kuibua vipaji kwani wamekuwa na mchango mkubwa sana katika michezo, MAMA Anna Kibira tumempoteza Ijumaa ya tarehe 4 Septemba, 2020 na Mzee Yasin Abdallah ametutoka leo tarehe 7 Septemba, 2020,” amesema Neema.