*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba imeanza vizuri Ligi Kuu baada ya kufanikiwa kuichapa Ihefu Fc mabao 2:1 katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Simba walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Mshambuliaji wao machachari John Bocco mnamo dakika 10 kwa kuachia mkwaju wa nguvu na kumuacha kipa wa Ihefu ashindwe la kufanya.
Bao hilo liliwafanya Ihefu Fc kuchangamka na kufanikiwa kusawazisha mnamo bao hilo dakika 14 kupitia kwa Omary Mponda.
Simba ilifanikiwa kuongeza bao la pili na kufunga mahesabu katika mechi hiyo kupitia kwa kiungo wao Mzamiru Yassin dakika 43 na mpira kumalizika dakika ya 90 kwa Simba kushinda Mabao 2:1