Home Mchanganyiko DKT.AKWILAPO AZINDUA MAFUNZO YA UMAHIRI WA UFUNDI WA SIMU ZA MKONONI

DKT.AKWILAPO AZINDUA MAFUNZO YA UMAHIRI WA UFUNDI WA SIMU ZA MKONONI

0

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Josephat Maganga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dkt Binilith Mahenge ,akizungumza wakati wa  hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA Mhandisi Pancras Bujulu,akitoa taarifa katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Bw.Samson Mwela akizungumza wakati wa  hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mkuu wa chuo cha Teknolojia Dar es Salaam(DIT)  Prof. Preksedil  Ndomba,akizungumza wakati wa  hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mwenyekiti mafundi simu mkoani Dodoma Emmanuel Msangi akielezea jinsi baadhi ya a mafundi simu zaidi ya 200 mkoani Dodoma waliopata mafunzo hayo.

Mwenyekiti wa mafundi simu Kanda ya Ziwa  Maguha Manyanda  Butonyole akitoa neno wakati wa  hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizindua  mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo,akimkabidhi Kitabu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Mhandisi Pancras Bujulu mara baada ya kuzindua   mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo,akimkabidhi Muongozo wa Kitabu Mkuu wa chuo cha Teknolojia Dar es Salaam(DIT)  Prof. Preksedil  Ndomba  mara baada ya kuzindua   mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwa katika picha mbalimbali za pamoja mara baada ya kuzindua  mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo iliyofanyika leo jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amezindua mafunzo ya umahiri wa ufundi simu za mkononi pamoja na mtaala wa mafunzo hayo.

Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. amewataka mafundi hao kuzingatia mafunzo yatakayotolewa ili wakafanye kazi kwa weledi na kujitengenezea ajira na uchumi wao,badala ya kufikiria kupata leseni na cheti pekee.

Hata hivyo Dkt.Akwilapo amewataka kufikiria zaidi kujiendeleza baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya VETA ambayo yatatolewa kwa wiki tano kwa ufadhili wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

“Lakini takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha watumiaji wa simu za mkononi walikuwa milioni 17,takwimu za sasa zinaonyesha watumiaji hao wamefikia milioni 48 hivyo wigo wa Mawasiliano unaendelea kupanuka.”amesema Dkt.Akwilapo

Aidha Dkt.Akwilapo ametoa wito kwa taasisi zingine kushirikiana na VETA katika kuwezesha mafunzo ya mafundi simu  huku akiwaasa wanufaika mafunzo kutoishia kwenye mafunzo na vyeti bali wawe chachu ya kuboresha huduma .

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA Mhandisi Pancras Bujulu amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuongeza tija na kuinua zaidi uchumi wa viwanda kupitia tehama.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA John Daffa amesema TCRA imeanzisha mitaala wa mafunzo simu ili kurasimisha shughuli za utengenezaji simu  na  kupunguza wimbi la.wizi wa simu za mkononi.

Mkuu wa chuo cha Teknolojia Dar es Salaam(DIT)  Prof. Preksedil  Ndomba amesema kuwa DIT imejipambanua kuwa taasisi ya Elimu ya juu katika Teknolojia na kuwaasa kusoma kwa bidii.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Josephat Maganga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dkt Binilith Mahenge amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia vijana kujiajiri wenyewe 

Mwenyekiti mafundi simu mkoani Dodoma Emmanuel Msangi amesema kuna mafundi simu zaidi ya 200 mkoani Dodoma waliopata mafunzo lengo ni kupanua wigo wa ajira kwa vijana huku Mwenyekiti wa mafundi simu Kanda ya Ziwa  Maguha Manyanda  Butonyole akisema kuwa kuanzishwa kwa Chama cha mafundi simu kumebadilisha Maisha yao .