Home Siasa WAGOMBEA MULEBA KUSINI WAJINOA VIKALI

WAGOMBEA MULEBA KUSINI WAJINOA VIKALI

0
 
Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Muleba Kusini Dr Oscar Kikoyo baada ya kupokea Ilani ya UchaguzI ya chama hicho kutoka kwa Mwenyekiti wa Mkoa Costancia Buhiye na kuhaidi kuinadi kwa wananchi.
 ***
Na Ashura Jumapili,Muleba
Wagombea wa Jimbo la Muleba Kusini katika nafasi ya Ubunge na Madiwani wameanza kunoa makali kupitia mikutano tofauti ya awali kabla ya uzinduzi rasmi wa kampeni utakaofanyika kesho siku ya Jumamosi Septemba 6,2020.
 
Mgombea Ubunge kupitia CCM Dr.  Oscar Kikoyo kwa nyakati tofauti ameshiriki mikutano iliyomkutanisha na wagombea wengine wa Ubunge na Udiwani kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanyika katika uwanja wa Zimbihire mjini Muleba.
 
Katika uzinduzi wa kampeini ngazi ya Mkoa Dr. Kikoyo alihaidi kuinadi ilani ya CCM inayotoa mwelekeo wa ongezeko la miradi ya maendeleo na kutoa ufumbuzi wa changamoto zilizobaki katika awamu ya kwanza ya uongozi wa miaka mitano wa Rais John Magufuli.
 
Akiwa katika Kata ya Nshamba Dr. Kikoyo aliahidi kushirkiana na diwani wa Kata hiyo na wadau wengine kupata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la uhaba wa maji na kuinua elimu hasa ujenzi wa shule za kidato cha tano na sita katka Jimbo hilo.
 
Mkutano huo pamoja na viongozi mbalimbali pia unatarajiwa kupambwa na wasanii kutoka ndani na nje ya Wlaya ya Muleba ambapo wagombea udiwani wote wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo.
Mgombea Ubunge wa Muleba Kusini Dr Oscar Kikoyo akihutubia wananchi wa Kata ya Nshamba eneo la Muznga na kuwahaidi kasi ya maendeleo.
Baadhi ya wanachama na mashabiki wa CCM katika mkutano wa kampeni Kata ya Nshamba Jimbo la Muleba Kusini.
Mgombea Udiwani Kata ya Nshamba Gosbert Masilingi akijinadi kwa wananchi wa Kata hiyo kuomba achaguliwe tena kutekeleza ilani ya chama chake.
Mgombea Udiwani kata ya Kibanga Edson Issaya akinadi ilani ya CCM na mgombea wa chama hicho katika Kata ya Nshamba Gosbert Masilingi.
Mgombea Ubunge Muleba Kusini Dr Oscar Kikoyo akijadili jambo na baadhi ya wananchi baada ya mkutano katika eneo la Muzinga Kata ya Nshamba.
Mjumbe wa NEC kutoka Mkoa wa Kagera Wilbroad Mutabuzi akitoa nasaha kwa wagombea waliopita kwenye uteuzi wa vikao vya chama kunadi mafanikio ya awamu iliyopita na ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
Mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Mazinga iliyoko kwenye Ziwa Victoria Edson Alex akiwa tayari kusaka kura zake na wagombea wengine baada ya kukabidhiwa ilani na vitendea kazi vingine.
Mgombea udiwani kata ya Kishanda Helmes Mushumbusi akisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika Kata ya Nshamba