Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa mkoa wa Singida kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bombardier uliopo Singida Mjini.
(PICHA IKULU NA JOHN BUKUKU-SINGIDA)
…………………………………….
Mgombea wa Urais Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Pombe Magufuli amesema serikali imetumia zadi ya Sh Bil 310 kujenga miundombinu wezeshi kiuchumi, miradi ya umeme nchi nzima, tumejenga madaraja, barabara na miradi mikubwa ya barabara ya Manyoni, Itigi hadi Chaya. Pia barabara ya Chaya hadi Tabora urefu wa kilomita 85 zimebaki kilomiga 20. Daraja la Sibiti halikuwepo. Ilikuwa changamoto kwa wananchi.
Dk. Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Bombadier mjini Singida amesema serikali metumia Sh Bil 17 kujenga barabara, “wasione vyaelea vimeundwa” Ameongeza.
“Nitawashangaa watu ikiwa watasimama katika mataa haya waseme watu waliozijenga. Wanamtukana Magufuli wakisimama katika barabara za Singida”.Alisema.
“Barabara kutoka Singida hadi Babati na Singida hadi Mwanza ilikua ndoto, barabara ya Singida hadi Dodoma urefu wa kilomita 245 haikuwepo watu waliteseka wanalala njiani. Pia barabara ya Mkiwa nataka iunganike na Mbeya nayo tutaichapa tu.”
Alibainisha kwamba ndio mana amekwenda kuwaomba kura wananchi wa Singida ili akaendeleze mahali palikobaki, anajua pesa zipo na watapanga wapi pa kuzitoa nyingine na ilani ya uchaguzi kurasa zote zinazumgumzia maendeleo.
Fedha zaidi ya Bil 479.4 kutekekeza miradi ya maendeleo Singida, hawakukopa pesa nje ni za wananchi zilizokuwa zinachezewa zinaliwa na mafisadi wamewabana sasa zinawaletea maendeleo Watanzania.
“Kwenye madini tulikua tunaibiwa na walijitokeza Watanzania kuwatetea. Nilipoingia madarakani vijiji
2018 tu vilikua na umeme, sasa vijiji 9570 vina umeme kati ya vijiji 12289 vilivyopo Tanzania yaani vimebaki vijiji 2600 na haviwezi kutushinda ndani ya miaka mitano vyota vitakua na umeme”Ameongeza Dk. Magufuli.
“Sisi tunataka maendeleo kwa Watanzania bila kubagua dini, makabila au vyama ndio maana tunawaomba mtupe kura.
Najua wapo wanaotaka tuingie kwenye matatizo lakini tutashinda maana kinachohitajika ni maendeleo ya kweli, haya yanahitaji uongozi wa kweli tunataka taifa hili liendelee kwenda mbele.”
“Tumeshaweka mikakati mizuri tumeshajenga bwawa la umeme kwa tumia Sh Trilionin 6.5 tunajenga kwa pesa zetu, umeme utakuwepo nchi nzima, tumeanza kusahau umeme wa mgao kwa sababu mliowachagua wametimiza wajibu wao. Ndio mana nawaomba kura Watanzania wote bila kujali vyama na hata ambao hawana chama kwa sababu maendeleo hayana chama.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Bombardier uliopo Singida Mjini.
Nyomi la Wananchi katika mkutano wa Kampeni wa CCM katika uwanja wa Bombadier Mjini Singida.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa Bombardier uliopo Singida Mjini kwa ajili ya mkutano wa Kampeni za Urais za Chama cha Mapinduzi CCM