Home Mchanganyiko MKUTANO WA 17 WA JUMUIYA YA WAHANDISI NCHINI KUFANYIKA JIJINI DODOMA

MKUTANO WA 17 WA JUMUIYA YA WAHANDISI NCHINI KUFANYIKA JIJINI DODOMA

0

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya maadimisho ya Siku ya Wahandisi kwa mwaka huu, Profesa  Mwinyiwiwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya siku hizo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 mwezi Septemba, 2020 jijini Dodoma.

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi, akifafanua jambo kwa   waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akizungumzia kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wahandisi yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 mwezi Septemba, 2020 jijini Dodoma.

………………………………………………………………

Na. Alex Sonna, Dodoma

Mwenyekiti wa maandalizi ya mkutano wa 17 wa Jumuiya ya Waandisi nchini, Profesa Bakari Mwinyiwima amesema kuwa wahandisi  zaidi ya 3,000 watashiriki moja kwa moja , zaidi ya 2,000 watashiriki kwa njia ya matandao mkutano huo.

Prof.Mwinyiwima ameitoa leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mkutano huo unaotarajiwa kuanza tarehe 3 na 4 mwezi Septemba, 2020 jijini Dodoma.

Aidha Prof. Mwinyiwima amesema  kuwa katika mkutano huo wahandisi 550 wanatarajia  kula kiapo cha utii ili kwernda kutekeleza weledi wao kwa ufasaha.

Prof. Mwinyiwima ameeleza kuwa Mkutano huo Bodi ya usajili wa wahandisi imewaalika viongozi wa ngazi za juu serikalini, mashirika ya umma na binafsi, wageni kutokna nje, wahandisi, makandarasali, wasanifu na wabunifu majenzi, wanafunzi wanaosoma uhadisi na wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu.

“Miongoni mwa wageni wa kimataifa watakao shiriki katika mkutano huo ni kutoka mataifa ya wageni wanaotarajia kushiriki ni kutoka Zimbabwe, Kenya, Nigeria, Uganda, Rwanda, Misri, Malawi, Botswana na Kenya”,.

Hata hvyo Prof.Mwinyiwima ameweka wazi kuwa mkutano huo utajadili mada kuu ya mapinduzi ya nne ya viwanda katika kufikia Malengo endelevu ya dunia: changamoto na fursa kwa wahandisi utakuwa na manada nyingine 10 ambazo zitaelezea mchango wa tekinolojia kutela tija kwenye kazi ya kiuhandisi.

Pia amesema kuwa watatoa  tuzo kwa taasisi zilizotia fora kwenye maonesho ya teknolojia na ubunifu, maonesho ya biashara, maonesho ya huduma za kitaaluma na maonesho ya uchuuzi

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Patrick Barozi amesema kuwa mpaka sasa wahandisi 29,019 wamesajiliwa na Bodi hiyo.