Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Manyoni katika Kampeni za Urais wakati akiwa njiani kuelekea Singida mjini .(PICHA NA IKULU)
……………………………………………………….
Na. Majid Abdulkarim, Manyoni
Mgombea Urais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa iwapoatachaguliwa kwa rais atahakikisha anakamilisha vijiji 2600 vinapatiwa umeme ili kumlika maisha ya watanzania.
Hayo ameyabainisha leo Wilayani Manyonyi wakati akielekea katika mktano wa kuomba kura mkoani Singida ili kuteuliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Aidha Dkt. Magufuli ameeleza kuwa ili kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wakutosha ndani ya miaaka mitano aliamua kujenga bwawa la umeme litakalokuwa linazalisha meme wa kutosha nchini na mwingini wa kuuza kwa nchi jirani na nyingine za Afrika.
“Lengo letu ni khakikisha nchi yetu inakuwa ya kisasa ambavyo tunataka watanzania kutoka katika umasikini kwenda katika maisha mazuri ya kila siku “amesisitiza Dkt. Magufuli.
Hata hivyo Dkt. Magufuli amebainisha kuwa katika ilani ya Chama ya Uchaguzi wa mwaka 2020/2025 wamejipanga kutekeleza makubwa na kuleta amani katika taifa la Tanzania.
“Hivyo tusirudi nyuma wanamanyoni na watanzania wote kwa jumla, nipeni awamu nyingine nikafanye maajabu katika kuleta maendeleo ya taifa hili”, ametoa wito Dkt. Magufuli.