Home Siasa DKT.MAGUFULI ATAKA HOSPITALI YA WILAYA BAHI KUKAMILIKA KWA WAKATI

DKT.MAGUFULI ATAKA HOSPITALI YA WILAYA BAHI KUKAMILIKA KWA WAKATI

0

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akipokewa na mamia ya wananchi wakati akiwasili  wilayani Bahi mkoa wa
Dodoma kwa mkutano wa kampeni wa hadhara leo , ikiwa ni kituo chake cha kwanza toka azindue rasmi kampeni zake za
kugombea Urais(PICHA NA IKULU)
Wananchi wa Bahi waliojitokeza kumpokea Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli  wakati akiwasili  wilayani Bahi mkoa wa
Dodoma kwa mkutano wa kampeni wa hadhara leo ,
ikiwa ni kituo chake cha kwanza toka azindue rasmi kampeni zake za
kugombea Urais(PICHA NA IKULU) 

……………………………………………………..

Na. Majid Abdulkarim, Bahi-Dodoma

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli ametaka uongozi wa wilaya ya Bahi kukamilisha hospitali ya Wilaya hiyo ili wananchi wa Bahi kupata huduma za Afya katika hospitali hiyo.

Kauli hiyo ameitoa leo wilayani Bahi Mkoani Dodoma wakati akiomba kura za kuteliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu takao fanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Dkt. Magufuli ameeleza kuwa ndani ya miaka mitano ya ongozi wake ndani ya wilya ya Bahi wanajenga hospitali ya wilaya itakayokamilika hivi karibuni, wamejenga vituo vya afya vitatu vilivyo tumia kiasi cha shilingi bilioni 1.3.

Aidha Dkt. Magufli ameeleza kuwa iwapoatapata ridhaa ya kuwa rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ataendelea kuboresha hdma za afya , elimu na miundombinu katika wilaya hiyo ili wananchi wa bahi waweze knfaika na maendeleo ya kchakua kiongozi bora.

Dkt. Magufuli ameeleza kwa ndani ya miaka mitano wamefanyikiwa ksambaza meme katika vijiji 45 vilivyopo katika wilaya ya Bahi hivyo anatoa wito wa wananchi wa Bahi kuhakikisha wanamcagua tena ili kendelea kusambaza umeme katika vijiji ambavyo bado havijapatiwa umeme.

“Tumeweza kutoa kodi zisizo za msingi na niwambie wakulima kwa kama mazao yako hayazidi tani moja hutakiwi kulipia kodi , lakini tnakilomita saba za lami katika wilaya ya bahi bado hazija kamilika hivyo mkiniparidhaa ya kuongoza ntakwenda kuzikamilisha na kuhakikisha mnapata barabara ili kuweza kusafirisha mazao yenu kiuraisi”, amesema Dkt. Magufuli.

Akihitimisha Dkt. Magufuli ametoa wito kwa wananchi wa Bahi kumchaga Mbunge wa Bahi Keneth Noro kuwa Mbnge wa Bahi, na kuchagua madiwani wa CCM kwa wingi ili kuleta karib wa kwatmikia wananchi hao.