…………………………………………………………
Na Pius Ntiga, Bahi
Amsha Amsha Dodoma leo imeongia siku ya Pili ikilenga kuainisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati pamoja na mafanikio ya serikali ya awamu ya tano, ambapo katika wilaya ya Bahi suala la changamoto ya maji linatajwa kuwa historia kutokana na limekuwa likitatuliwa kadri inavyowekezeka.
Wilaya ya Bahi inajumla ya vijiji 59 na wakazi 271,069 ambapo katika mafanikio miongoni mwa wananchi wameaifu hatua ya serikali kutatua suala la maji Safi na salama ambalo lilikuwa ni changamoto kwao.
Mwanahamis Munkunda ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi ambaye ameiambia Uhuru FM kuwa Wilaya ya Bahi siyo Ile tena ya miaka iliyopita.
Asilimia 4 nukta 5 ya wakazi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi wana umri wa miaka 65 au zaidi na Wilaya hii imeanzishwa zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Kuhusu suala la Maji takwimu zinaonesha kuwa Kati ya vyanzo vya maji vilivyoripotiwa, visima vifupi vya maji ni 96 kuliko vyanzo vingine ikifuatiwa na mashimo 54 na uvunaji wa mji ya mvua Ni 24.
Kuhusu suala ya vitambulisho Elfu 45 vimepokelewa Awamu ya Pili katika Wilaya hiyo ili wafanyabiashara wadogo afanye Biashara zao katika mazingira rafiki.
Kuhusu suala la umeme amesema vijini 42 tayari vimeshawashwa umeme kati ya vijiji 59 na vilivyobaki vitaunganishwa na umeme kupitia REA kabla ya kumalizika mwaka 2020.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi Dkt Fatuma Mganga ameainisha miradi ya kimkakati katika Halmashauri hiyo kuwa imetekelezwa kwa asilimia 90 na wananchi amesema wamekuwa na Imani na serikali yao.
Miundombinu katika elimu madarasa Mia Saba yameongezwa ikiendana na ongezeko la wanafunzi kupitia Mpango wa elimu bila malipo kwa kipindi Cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Dkt Mganga amesema Asilimia 78 ufaulu shule ya msingi umeongezeka kutoka asilimia chini ya 28.
Kuhusu uchumi kipato amesema Pato la mwananchi mwanzo lilikuwa laki nne na ishirini ambapo sasa limefika milioni moja hii ni kutokana na kazi za kiuchumi zinazofanywa na wananchi wa Bahi.
Kuhusu kilimo na mifugo amesema hali iliyopo Sasa ni tofauti na miaka mitano iliyopita kwani Biashara ya Mifugo imeongezeka huku Kilimo kikichangia zaidi uchumi wa Bahi kupitia kilimo Cha Mpunga.
Shilingi Bilioni Moja ni mapato ya Halmashauri yameongezeka hii ikiwa ni uwajibikaji wenye tija wa Halmashauri ya Bahi.
Amesema pia wamefanikiwa kutoa Mikopo shilingi Milioni 90 kwa makundi ya vijana na Akinamama hii ikiwa Ni kutokana na mapato ya ndani.
Dkt Mganga amesisitiza kuwa Majosho sita ya Mifugo yamekarabatiwa na yamepunguza vifo vya mifugo na pia wanampango wa kutengeneza Stendi ya Wilaya ya Bahi kupitia mapato yao.
Aidha kupitia serikali kuhamisha Makao Makuu ya nchi kuwa Dodoma amesema wananchi watanufaika kupitia Soko la Mchele na Nyama.
Pia Wilaya ya Bahi ipo katika mchakato wa kuanzisha Kiwanda cha Ngozi.
Kuhusu Viwanja amesema vipo katika sehemu nzuri na inafikia vizuri hivyo amewaomba wananchi kuchangamkia viwanja Bahi.
Kutokana na mafanikio hayo wamewaomba wananchi wa Bahi kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi wa mwaka huu ili viongozi waendeleze mafanikio makubwa yaliyopatikana.