Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Thamani kwa Wateja Vodacom Tanzania PLC, Jackson Walwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu bando jipya la Vodacom Jimixie linalowapa wateja uhuru na urahisi wa kujitengenezea mseto wa bando zao wenyewe kutegemeana na mahitaji yao, muda wa kuisha kwa bando, motisha na gharama. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa.
Wafanyakazi wa Vodacom, wateja na wanahabari wakifuatilia tangazo la JIMIXIE BUNDLE lililokuwa likichezwa kwenye screen wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya kutoka mtandao wa Vodacom.
……………………………………………………..
Huduma hii mpya inalenga kuwawezesha zaidi wateja.
Dar es salaam.
Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali nchini, Vodacom Tanzania PLC leo imezindua huduma nyingine ya kwanza na ya kipekee katika soko ijulikanayo kama Jimixie bando – Hii ni huduma ambayo inawapa wateja uhuru na urahisi wa kujitengenezea mseto wa bando zao wenyewe kutegemeana na mahitaji yao, muda wa kuisha kwa bando, motisha na gharama.
Akiongea na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo
mpya, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Bi Linda Riwa amesema, kwa miaka mingi kampuni
ya Vodacom imeonyesha mfano katika uvumbuzi na kujenga jamii ya kidijitali kwa kuzindua
huduma za pekee na za kwanza sokoni kwa sababu ya ari ya kampuni hii ya kufanya maisha ya
wateja kuwa rahisi, bora na yenye utoshelevu zaidi kwa kupitia teknolojia na uvumbuzi.
“Kwa kutambua kwamba mahitaji ya kila mteja ni tofauti na wakati huo huo wateja wote
wanahitaji kupata thamani zaidi kwa kile wanachokilipia, tumeamua kutengeneza huduma
ambayo inawapa uhuru wa kupata kile wanachohitaji na kwa gharama ambayo wako tayari
kuilipa. Mteja anaweza akatengeneza bando lake mwenyewe lenye Data, SMS na Dakika za
maongezi kwa pamoja kutegemeana na mahitaji yao, kwa gharama wanayoweza kuimudu na kwa
muda wa kuisha kwa bando wanaoutaka. Huu ni ushahidi wa namna ambavyo tunawajali wateja
wetu kwa kuwapatia uhuru wa kutengeneza mseto wa bando zao wenyewe jambo ambalo
litawapa urahisi na uhakika katika namna ambavyo wateja wanafanya matumizi yao” alisema
Riwa.
Vodacom Tanzania PLC inajivunia kuwa kampuni inayomjali mteja huku ikiwa na aina
mbalimbali za bando ambazo zinakidhi mahitaji ya wateja kutegemeana na mahitaji yao mahsusi.
Hata hivyo ni mara ya kwanza kampuni hii inaruhusu wateja wake kujitengenezea bando zao
wenyewe kwa gharama yoyote wanayoweza kuimudu ili kuweza kupata kile wanachohitaji.
“Kwa mara ya kwanza nchini, wateja watakuwa na uwezo wa kuchagua ni kiasi gani wanataka
kutumia, na wanataka kutumia katika huduma gani. Tutaendelea kuzindua huduma zenye ubunifu
kwa wateja wetu ili kuhakikisha kwamba wanapata huduma za kipekee kwenye mtandao bora na
wa kisasa popote pale walipo wakiwa na Vodacom. Tumefanya hivi kwa ajili ya kurahisisha
maisha ya wateja wetu tukiwapa uhuru wa kununua kile wanachotaka kutumia huku wakipata
manufaa zaidi katika Data, SMS na matumizi ya dakika za muda wa maongezi,” alihitimisha Riwa.
Akiongelea kuhusu utaratibu wa huduma, Mkuu wa idara ya Mikakati na Thamani kwa Wateja
Jackson Walwa amesema kwamba huduma hii inapatikana kwa wateja wote na katika mifumo
yote ya simu za kawaida na simujanja kwa kupiga kupiga *149*01#J4U>JIMIXIE BUNDLE,
Mteja atakuwa na uwezo wa kutengeneza bando lake mwenyewe kutegemeana na anataka nini na
huduma anayoweza kuimudu.
“Huduma ya JIMIXIE BUNDLE imetengenezwa mahususi kuhakikisha kwamba wateja wetu
wote wanaweza kununua bando bila kujali wana kiasi gani; unaweza kununua bando kwa kiasi
C1: VODACOM PUBLIC
kidogo cha fedha cha TSH 520, TSH 630, TSH 710, TSH 870 au ukiwa na kiasi chochote cha juu
unachotaka. Kwa kifupi hatumuachi mtu nyuma,” alisema Walwa.
Kuhusu Vodacom Tanzania:
Vodacom Tanzania PLC ni watoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi na watoa
huduma za kifedha kupita simu za mkononi wanaoongoza. Tunatoa huduma mbalimbali za
mawasiliano kwa wateja na makampuni – ikiwemo sauti, data na ujumbe mfupi, video, cloud
hosting, masuluhisho ya simu za mkononi na huduma za kifedha – kwa zaidi ya wateja milioni
14.1. Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Kundi la
makampuni ya Vodacom (Vodacom Group) iliyosajiliwa Afrika Kusini, ambayo kwa upande
mwingine inamilikiwa na kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya
Vodacom imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwa namba ISIN:
TZ1886102715 Stock name: VODA.
Kwa taarifa zaidi , tafadhali tembelea tovuti: www.vodacom.co.tz