Home Siasa KATA 30 ZA MKOA NA JIMBO MOJA LA LUDEWA ZAKATIWA RUFAA

KATA 30 ZA MKOA NA JIMBO MOJA LA LUDEWA ZAKATIWA RUFAA

0

NJOMBE

Chama cha demokrasia na maendeleo chadema mkoa wa Njombe kimesema kimewasilisha mapingamizi 30 kwa wazimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata na halmashauri ambazo zimewaondolea sifa ya kuteuliwa wagombea wao wa nafasi za ubunge na udiwani katika maeneo tofauti.

Akizungumza na vyombo vya habari mwenyekiti wa chadema mkoa Rose Mayemba amesema katika kata 107 za mkoa wa Njombe , wagombea 30 wa ngazi ya kata wameondolewa kwa madai ya kukosa sifa za kuteuliwa kugombea udiwani huku kwa ngazi ya ubunge mgombea jimbo la Ludewa Ndugu James Haule akidaiwa kuondolewa baada ya msimamizi wa uchaguzi kutilia shaka sahihi ya katibu wa jimbo wa chama.

Kuhusu madiwani waliokosa sifa mwenyekiti huyo amesema kuna wagombea walioondolewa kwa madai ya kukosea kujaza fomu , kuvamiwa na kuibiwa fomu pamoja na kutekwa kwa baadhi  ya wagombea na kushindwa kurejesha fomu kwa wakati.

Mayemba amesema katika majimbo mawili likiwemo la Makambako na Makete wagombea wote wa ngazi ya udiwani na ubunge wametauliwa lakini majimbo mengine manne ambayo ni Wanginbaadhi ya wagombea wameondolewa kwasababu mbalimbali

Akifafanua mwenendo wa uteuzi katika kata zote 107 Mayemba amesemma Katika majimbo ya Makete na Makambako wagombea wote wa ubunge na udiwani wameteuliwa huku katika jimbo la Ludewa lenye kata 26 wagombea 16 wameondolewa pamoja na mgombea mbunge, Lupembe yenye kata 12 mgombea wa kata 1 ameondolewa, Wanging’ombe yenye kata 21 wagombea 10 wameondolewa huku jimbo la Njombe mjini lenye kata 13 mgombea 1 amekosa sifa.

Kufuatia malalamiko hayo mtandao huu umelazimika kumtafuta msimamizi mkuu wa uchaguzi mkoa wa Njombe Mwanasheria Hilmar Danda kujua kama amepokea pingamizi lolote hadi sasa jambo ambalo linakanushwa kwa kudai kwamba huenda bado yapo ngazi ya nchini huku akisema itafahamika ifikapo saa kumi jioni.

Sakata hilo pia limelazimu kuzungumza na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa kujua kama kuna kesi zilizoripotiwa kuhusu uvunjifu wa kanunu na taratibu za uchaguzi ikiwemo uvamizi na utekaji ,tuhuma ambazo zimekanushwa na kamanda huyo ambaye anasema yupo wilayani Makete kikazi hivyo anaendelea kufatilia kwa karibu ili uchaguzi ufanyike kwa huru na kaki.