Injinia Emmanuel Kalobelo Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro akifungua semina ya wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Mpango wa Tatu wa Kunusuru kaya masikini inayofanyika Chuo Cha Veta mkoani Morogoro katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa (TASAF) Bw. Ladslaus Mwamanga na Selina Wilson Mwenyekiti wa Semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa (TASAF) Bw. Ladslaus Mwamanga akimkaribisha Injinia Emmanuel Kalobelo Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro kulia ili kufungua semina ya wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Mpango wa Tatu wa Kunusuru kaya masikini awamu ya pili inayofanyika Chuo Cha Veta mkoani Morogoro kushoto ni Selina Wilson Mwenhyekiti wa semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa (TASAF) Bw. Ladslaus Mwamanga kushotona Injinia Emmanuel Kalobelo Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro wakifuatilia kwa karibu mjadala uliokuwa ukiendelea katika semina hiyo.
Zuhura Mdungi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TASAF akitoa maelezo kwa washiriki wa semina hiyo kabla ya kuanza kwa semina.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Dismas Mwakwinja Afisa Ufuatiliaji na Udhibiti wa Kero TASAF akitoa ratiba ya semina hiyo kabla ya kuanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa (TASAF) Bw. Ladslaus Mwamanga akiwasilisha mada kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari katika semina iliyofanyika kwenye Chuo cha VETA mjini Morogoro.
Injinia Emmanuel Kalobelo Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro akisalimiana na Mhariri wa gazeti la Uhuru Selina Wilson.
Injinia Emmanuel Kalobelo Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro kushoto akiongozana na Mhariri wa Mwananchi Angetile Osiah na Godwin Harrison Mkisi kulia Kaimu Mkuu wa Fedha na Utawala.
Faraj Mishael Mtaalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini TASAF akiwasilisha mada katika semina hiyo.
Amadeus Kamagenge Mkurugenzi Miradi ya Huduma za Jamii TASAF akifafanua jambo katika semina hiyo.
Picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwaseminahiyo.