Katika Halmashauri ya Wilaya ya kibaha vijijini Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nuru Ndalahwa amesema wamefanikiwa kutekeleza miradi yenye thamani ya mabilioni ya fedha hasa katika sekta ya Afya, Maji na Miundombinu na wananchi wameonesha kusifu mafanikio hayo.
Katika Afya wamefanikiwa kupunguza idadi ya vifo walivyokuwa wakipata akinamama wajawazito baada ya kujenga kituo Cha afya kwa zaidi ya shilingi bilioni moja ambacho kitakuwa na Hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya kwa kuweka vifaa vya kisasa katika chumba Cha kujifungulia.
Pia mafanikio mengine Ni kushawishi wananchi kujiunga katika bima ya Afya sanjari na kuwakatia vitambulisho kwa ajili ya matibabu bure kwa wazee.
Akisungumzia Hali ya elimu amesema Asilimia 92 ufaulu umeongezeka katika Halmashauri ya kibaha mjini kwa kuwa na shule zaidi ya 37 za serikali na shule nane watu binafsi na kuwa na idadi kubwa ya walimu.
Kwara shule ya msingi ipo eneo ambalo amesema limezungukwa na wafugaji kumejengwa shule ya msingi na imeondoa changamoto ya watoto kutokenda kuchunga mifugo na badala yake Sasa wanakwenda shule ya msingi.
Shilingi bilioni tatu elimu bila malipo kila mwisho wa.mwezi kiasi hicho Cha fedha wamekuwa akipokea kutoka serikali kuu na Hali hiyo amesema imechangia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wanafunzi katika Halmashauri ya kibaha vijijini.
Kuhusu changamoto waliyo nayo katika shule za sekondari Ni kutokuwa na walimu wa kutosha wa Masomo ya sayansi, hivyo ameiomba serikali kuliangalia eneo Hilo kwa kuleta walimu wa masomo hayo.
Kuhusu ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya kibaha vijijini zaidi ya shilingi bilioni mbili zimetolewa na serikali kujenga ofisi ya Halmashauri katika mji wa mlandizi na ujenzi umeanza.
Kuhusu fursa zipo katika eneo la uwekezaji amewaomba wananchi waende eneo la kwala kwani kupitia bandari kavu katika eneo Hilo watanufaika na uwekezaji kupitia ujenzi pia wa Nyumba za kulala wageni.
Kuhusu suala la migororo ya Ardhi wamejitahidi kuitatua kadri inavyowafikia katika Halmashauri hiyo na mgogo uliopo ni kati ya Halmashauri ya kibaha mjini na morogoro ambao tayari wameufikisha tamisemi kwa ajili ya kuitatua