Waandishi wa Habari na wakifuatilia Semina ya Wataalamu wa Ustawi wa Jamii (TASWO) na waandishi wa habari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Ustawi wa Jamii (TASWO) akizungumza katika Semina ya Wataalamu wa Ustawi wa Jamii (TASWO) na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Stella Msofe akizungumza katika Semina ya Wataalamu wa Ustawi wa Jamii (TASWO) na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
**********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Waandishi wa habari nchini,wametakiwa kuripoti matukio yanayohusu makundi maalumu kwenye jamii kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na kwa kufuata sheria ili kuepuka uzalilishaji na kuhifadhi utu wao.
Wito huo umetolewa leo na katibu tawala wa Wilaya ya Kinondoni Stella Msofe wakati wa ufunguzi wa Semina ya wataalumu wa ustawi wa jamii (TASWO) Na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Stella amesema kuwa kuna muda yanapoendewa makundi maalumu ya watu kwenye jamii wanahabari husau baadhi ya maadili ya kazi na baadae kusababisha uzalilishaji hivyo kupitia semina hiyo anatarajia itakuwa chachu ya mabadiliko kwa wanahabari.
“Chombo cha habari ni muhimu sana hapa nchini kwani kinaweza kujenga ama kubomoa nchi,wenzetu wa TASWO wameliona hilo na kulifanyia kazi ni wapongeze sana,serikali inaunga mkono juhudi zao za kuelimisha umma”. Amesema Mhe.Stella.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa ustawi wa jamii nchi (TASWO) Dkt. Mariana Makuu amesema mara nyingi waandishi hutoa taarifa kwa nia nzuri ya kuwasaidia waathirika wa matukio mbalimbali lakini uwasilishaji wake unaweza kuleta maumivu makubwa baadae.
Aidha Dkt.Mariana ameongeza kuwa uripotiji wa matukio ya makundi maalumu kama vile watoto,wakimbizi na walemavu yasipozingatia misingi ya maadili na utu huweza kusababisha muhusika kutengwa,kunyanyapaliwa,kukosa baadhi ya haki za msingi na kunyanyaswa kutokana na picha,video ama habari fulani iliyoripotiwa kwenye mitandao na vyombo mbalimbali vya habari.
“Ipo haja ya kuangalia namna nzuri ya kuwasaidia makundi maalumu na waathirika wa majanga ili kuwaacha wakiwa salama”.Amesema Dkt.Mariana.