Mshambuliaji Andrew Simchimba akishangilia baada ya kuifungia Azam FC bao la ushindi dakika ya 66 ikiwalaza Namungo FC 2-1 katika mchezo wa kirafiki kwenye kilele cha Tamasha la Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Azam FC ilitangulia kwa bao la Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 37 kabla ya Mghana Steven Sey kuisawazishia Namungo FC dakika ya 57.