Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi jimbo la Biharamulo Mhandisi Ezra John Chiwelesa Kulia akipokea fomu ya kugombea ubunge kutoka kwa mkurugenzi wa uchaguzi wa wilaya ya Biharamuro Wazir Kombo katika ofisi za tume ya uchaguzi Agosti 22, Mwaka huu. Mhandisi Ezra John Chiwelesa mgombea ubunge jimbo la Biharamulo kwa tiketi ya CCM akiongea na wanaccm pamoja na wananchi waliojitokeza kumshangilia katika ofisi za CCM Wilaya Biharamulo. Mgombea ubunge jimbo la Biharamulo Mhandisi Ezra John Chiwelesa Akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya waliokuwa watia nia wenzake katika kinyanganyiro cha kura za maoni waliojitokeza kumdhamini.
Waendesha pikipiki, wanachama wa CCM na wananchi wakiwa kwenye msafara wa kumpokea mgombea ubunge wa jimbo la Biharamulo Mhandisi Ezra Chiwelesa akitoka kuchukua fomu ya kugombea kwenye ofisi za tume.
Picha zote na Allawi Kaboyo Biharamulo.
**********************************
Na Allawi Kaboyo Biharamulo.
Baada ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi tarehe 20, mwezi huu kupitia kwa katibu wa itikadi siasa na uenezi wa chama hicho Hamphrey Pole pole kutangaza majina ya walioteuliwa kugombea nafasi za ubunge,uwakilishi na viti maalumu Aliyeteuliwa kugombea Biharamulo achukua fomu.
Akiongea baada ya kufika ofisi za tume leo Agost 22,mwaka huu, mgombea huyo Ndugu Ezra Chiwelesa amesema kuwa anakishukuru chama chake kwa kumuani na kumteua kukiwakilisha katika uchaguzi ujao ambapo ameongeza kuwa hata yeye hakutegemea kuipata nafasi hiyo licha ya kuwa katika kura za maoni alipata nafasi ya pili akiwa nyuma ya Dr.Gresmus Sebiyoya aliyeongoza kinyanganyilo hicho.
Ezra amesema kuwa sasa ni wakati wa wanabiharamulo kuungana na kuijenga biharamulo yao na kuongeza kuwa wagombea wote waliojitokeza kuomba kuteuliwa atashirikiana nao kwa mawazo na mambo yote.
“Nakishuru chama change kwa kuniteua, tulikuwa 51 ila kimeniona na kuniamini mimi sio kwamba nawazidi wenzangu au ninajua sana kuwazidi wenzangu ila ilikuwa apatikane mmoja. Nawashukuru watia nia wenzangu ambao pia wamejitokeza kunisindikiza na kunidhamini mimi nitashirikiana nao wote maana kila mmoja alikuwa na maono yake juu ya Biharamulo yetu.” Amesisitiza Ezra.
Ameongeza kuwa malengo yake ni kuhakikisha wilaya ya Biharamulo inaondokana na wimbi la umasikini kama inavyosemekana kuwa wilaya ya pili kutoka mwisho kwa umasikini, ambapo ameongeza kuwa kwa kushirikiana na wanabiharamulo anandoto ya kuibadirisha bihara mulo kwa Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara,maji n.k.
Kwaupande wake mkurugenzi wa uchaguzi wa wilaya hiyo ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashuari hiyo Wazir Kombo amesema zoezi la uchukuaji fomu kwa wagombea linaendelea vizuri kwa utulivu na Amani ambapo hadi kufikia tarehe 22/08/2020 majira ya saa tano asubuhi wagombea ambao walikuwa wamechukua fomu ni watano.
“Zoezi linaendelea vizuri na wala hatujakutana na changamoto yoyote hususani suala la usalama wagombea wote wamekuja kwa taratibu zilizoelekezwa na mpaka sasa nina vyama vitano ambavyo vimechukua fomu ambavyo ni CHADEMA, CUF,NCCR MAGEUZI, CCM na NLD nab ado tunaendelea kuwasubiri wagombea wengine kutoka vyama vingine maana vyama ni 19.” Amesema Wazir.
Dr.Gresmus Sebuyoya ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa na ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliotia nia ya kugombea ubunge wa jimbo hilo na katika kura za maoni yeye aliongoza kwa kupata kura Zaidi ya 400 amesema kuwa anaheshimu maamuzi ya chama na yupo tayari kwa namna yoyote kumuunga mkono mgombea aliyeteuliwa na chama chake kuwania ubunge katika jimbo hilo.
Ameongeza kuwa anayoimaani kubwa na Ezra kwa kuwa chama kimemuamini na kumteua sasa makundi yameisha sasa wanapambana kuhakikisha wanashinda uchaguzi mkuu ambapo ameongeza kuwa anakwenda kumdhamini kwenye fomu ya ugombea ubunge.
Aidha wananchi na wanachama wa chama wa CCM wamejitokeza katika barabara za mitaa ya mji wa Biharamulo na kusababisha baadhi ya Barabara hizo kufungwa kwa muda kwa lengo la kumshangilia mgombea ubunge wao huku wakiwa na shahuku ya kumsikiliza, ambapo vijana wa boda boda wakijitokeza kuandamana na kumsindikiza hadi nyumbani alipotoka ofisi za tume kuchukua fomu.