Mwenyekiti wa Jukwaa la Hedhi Salama Tanzania Bi. Salvata Silayo akitoa zawadi ya sabuni ya kusafishia vyoo kwa ajili ya shule hiyo.Wadau mbalimbali wa hedhi salama wakiwa kwenye ofisi ya mkuu wa shule ya msingi ya wasioona Buigiri iliyoko wilayani ChanwinoWadau mbalimbali wa hedhi salama wakiwa kwenye ofisi ya mkuu wa shule ya msingi ya wasioona Buigiri iliyoko wilayani Chanwino.
***************************************
Na. Catherine Sungura,WAMJW-Chamwino
Jukwaa la Hedhi Salama Tanzania limefanya tathimini ya mafunzo ya namna ya kujisitiri kwa wanafunzi wakati wa hedhi kwenye shule ya msingi ya wasioona Buigiri wilayani Chamwino.
Akiongea baada ya tathimini hiyo Mwenyekiti wa Jukwaa hilo ambaye pia ni Afisa Afya Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Salvatha Silayo amesema kuwa lengo la tathimini hiyo ni kuona jinsi walimu na wanafunzi hao walivyotekeleza kwa vitendo mafunzo waliyopatiwa mwaka jana shuleni hapo.
Bi. Silayo amesema kuwa mwaka 2019 jukwaa hilo ambalo linawajumlisha wadau mbalimbali wa hedhi salama lilitoa mafunzo kwa wanafunzi hivyo katika kipindi cha mwaka mmoja kimepita hivyo wameona ni vyema kufika shuleni hapo kuweka mikakati kwa pamoja na yale ambayo hayajaweza kutekelezwa kuweza kuyatekeleza na kuboresha zaidi kwa mustakabari wa kuwawezesha wanafunzi wa shule hiyo kutekeleza kwa ukamilifu bila vikwazo vyovyote.
“Mwaka jana tulifika shuleni hapa na kuwapatia wanafunzi wote na walimu wao namna ya kujisitiri wanapokuwa kwenye hedhi,hivyo tumekuja kuangalia je yale tuliyowafundisha wametekeleza,tumeona mambo mengi yametekelezeka na yale machache tumeyawekea muda yatekelezwe.
Naye Mlezi wa Wanafunzi shuleni hapo Bi.Clementina Njelima amesema kuwa wanafunzi wao ni wepesi sana kushika yale wanayofundishwa hivyo wanafunzi wote wanatekeleza kwa makini mafunzo waliyopatiwa kwani wameweka utaratibu mzuri kwa kuweka vifaa vya kuhifadhia taka kwenye bafu wanalotumia na pia kujenga kichomea taka shuleni hapo.
Mmoja wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo amesema kuwa mafunzo ya hedhi salama yamewasaidia kuwaondolea hofu miongoni mwao na hivyo wanapofika hatua hiyo wanakua wanaelewa namna ya kujisitiri na hivyo kuwajengea kujiamini na kufanya kuendelea na masomo yao kawaida bila woga wowote.