Viongozi mbali mbali wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani kati kati Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mkutano huo wa hadhara, kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani wakiwa wametulia na kufurahia jambo kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Pwani hayupo pichani wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na wananchi wa Kisarawe katika mkutano huo wa hadhara ambao uihudhuliwa na wananchi mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wakuu wa idara. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kulia akiagana kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kumalizika kwa ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kugagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliz akero na changamoto za wananchi. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo aliyesimama akizungumza na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Kisarawe katika mkutano wa adhara wakati wa zira yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea miradi mbai mbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na kushoto kwake ni waliokaa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa anakagua ubora wa vifaa ambavyo vinatumika katika utengenezaji wa madawati na meza kwa ajili ya wanafunzi mbali m,bali wa shule za msingi na sekondari Wilayani Kisarawe.Mmoja wa wazee maarufu wanaosihi Wilayani Kisarawe akisalimiana na Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Pwani mara baada yam zee huyo kumaliza kutoa kero na changamoto zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye alifanya ziara ya kikazi. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akipeana mkono na mzee mkongwe wa Wilaya ya Kisarawe wakati wa mkutano wa adhara ambao ulioandaliwa kwa ajili ya kuweza kusikiliza kero na changamoto mbali mbali za wananchi.
(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
***********************************
NA VICTOR MASANGU, KISAARAWE
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kwamba hawezi kuwavumilia watendaji na watumishi ambao ni wazembe na badala yake atahakikisha anawachukulia hatua kali ikiwemo kuwafukuza kabisa endapo watabainika hawatimizi wajibu wao ipasavyo kwa mujibu wa sheria kanuni na taribu zilizowekwa.
Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kutembelea na kukagua miradi mbali mbai ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wananchi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Pia Ndikilo aliwataka watendaji hao kuhakikisha wanatoka maofisini na kwenda kusikiliza changamoto na kero sinazowakabili wananchi hususan wa maeneo ya vijijini ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi haraka na sio kusubiia hadi kiongozi wa ngazi za juu afanye ziara ya kwenda kuzitafutia ufumbuzi wakati kuna wahusika ambao wanaweza kuzifanyia kazi.
“Ninawaagiza watendaji wote wa vijiji watendaji wa kata kuhakikisha kwamba mnazingatia mambo muhimu katika kazi zenu na kitu kikubwa ninashangaa sana kuona malalamiko yanakuwa ni mengi wakati nyinyi mpo hii ni aibu kabisa yani mpaka kiongozi mkubwa kutoka ngazi za juuu aje kuwasikiliza wananchi kero zao zinazowakabili wakati na nyinyi mpo kwa kweli hii sio sahihi kabisa hata kidogo,”alisema Ndikilo.
Aidha alisema kuwa kitukikubwa wananachotakiwa kukifanya watumishi kwa kushirikian ana watendaji ni kuweka ratiba zao za kwenda katika maeneo mbali mbali ya vijiji na vitongozi ili kuwasikiliza wananchi wanakabilia na changamoto gani na kuzishughulikia katika maeneo mbali mbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, miundombinu ya bara bara maji, umeme na mambo mengine ya kimaendeleo.
Ndikilo katika hatua nyingine alizitaka taasisi na mashirika mengine yasiyokuwa ya kiserikali kushirikiana kwa pamoja na serikali ya awamu ya tano ambayo inaongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa lengo la kuweza kukuza uchumi wa nchi sambamba na kuleta chachu ya kimaendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kwamba anachukizwa na kuona baaadhi ya watendaji wengine kutotimiza wajibu wao ipasavyo na kuwa mizigo hivyo amewataka wabadilike na kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuweza kuwatumikia wananchi mbali mbali.
Aidha Mwegelo alisema kwamba kumekuwepo na kesi mbali mbali zinazohusiana na migogoro ya ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa inasababisha na watenaji wa kijiji, watendaji wa vitongoji hivyo amewaonya kuachana na hali ni na kuwataka kushirikiana bega kwa began a wananchi wa maeneo husika na kutouza maeneo kiholela bila ya kuzingatia sheria.
“Kwa kweli kuna wakati mwingine hii migogoro inasababisha na baadhi ya watendaji wetu wenyewe maana mKuu wa Mkoa katika mkutano huu wa leo ukiangalia asilimia kiubwa malalamiko mengo ambayo yametolewa na wananchi hawa utaona ni dhahiri migogoro hii imetokana na baadhi ya watendaji wetu kwa hiyo mimi nataka hii hali isiwepo kabisa na ibadilike,”alisema Jokate.
Pia alisema kammba lengo kubwa la serikali ya Wilaya ya Kisarawe ni kuhakikisha inaweka mipango madhubuti ya kuweza kupunguza na kuondoa kabisa migogoro ya mipaka ya ardhi ili kila mwananchi aweze kuwa na hali ya amani na na kwamba wataendelea kuwaelimisha watendaji ili waweze kufatekeleza majukumu yao kwa weledi.
“Viongozi sisi tumepatatiwa dhamana kwa hivyo inabidi tuhakikishe kwamba tunamuunga mkono Rais wetu wa aawamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na ndio maana kwa upande wangu sipengi kabisa mtumishi aua mtendaji katika Wilaya hii ya Kisarawe aanakuwa ni mzigo kabisa hii hali siipendi,”alisisitiza Jokate.
Katiaka hatua nyingine ,Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika sekta ya elimu kwa sasa wameshaanza mikakati ya kutengeneza viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuhakiksha wanasoma katika mazingira yaliyo rafiki na kuondokana na hali ya kukaa kwa mlundikano.
Nao baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Kisarawe ambao walihudhuria katika mkutano huo walimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis Evarist Ndikilo pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo kwa kuweza kuamua kuwakutanisha kwa pamoja ili kuweza kuwapataia fursa ya kusikilia changamoto na kero amabzo zinawakabili ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo bado anandeleo na ziara yake katika Wilaya zote zilizopo mkoani humo ambapo kwa siku ya lo ameweza kufanya ziaara yake Wilaya ya Kisarawe na kutembelea baadhi ya maeneo ikiwemo kugagua kalakana ya kutengenezea viti na meza kwa ajili ya wanafunzi pamoja na kuzungumza na wananchi kutoka maeneo mbali mbali.