Home Mchanganyiko WAFUNGWA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

WAFUNGWA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

0

……………………………………………………….

Na.Mwandishi Wetu

Mahakama Kuu Kitengo cha uhujumu uchumi kanda ya Bukoba mnamo tarehe 17/8/2020 mbele ya Muheshimiwa jaji Lilian Mashaka kupitia shauri la uhujumu uchumi no 1/2020 la Jamhuri dhidi Paulo S/O Andrea @Mbwilande na John S/O Paulo imewakuta na hatia washtakiwa wote wawili kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo vipande vitatu , Sawa na tembo wawili yenye thamani ya USD 30 Sawa na Tsh 68,382,000/=.

Washtakiwa hawa walikamatwa na meno hayo ya tembo na askari wa Doria wa maliasili mnamo tarehe 22/07/2018 katika kijiji cha Nyamigere wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera.

Washtakiwa wamepewa adhabu ya Kulipa faini Tsh Mil 683,820,000/ au kwenda jela miaka 20 kila mmoja.

Washtakiwa wote walishindwa kulipa faini hiyo na kupelekwa gereza la wilaya ya Bukoba kutumikia vifungo vyao, Mbali ya adhabu hiyo pia mahakama ilitaifisha meno hayo ya tembo.

Katika hatua nyingine tarehe 18/8/2020 mahakama kuu kanda ya Bukoba mbele ya Muheshimiwa jaji Lilian Mashaka kupitia shauri la uhujumu uchumi no 2/2020 la Jamhuri dhidi Jasson Pascal na Antidius S/O Paschal imewakuta na hatia washtakiwa wote wawili kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo yenye thamani ya Tsh 33,780,000/=na kuwapa adhabu ya kulipa faini Tsh mil 337 ,800,000/= au kwenda jela miaka 20.

Washtakiwa Hawa walikamatwa na askari wa jeshi la polisi mnamo tarehe 4/4/2018 katika kijiji cha Bimulo wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera wakiwa na nyara hizo za serikali.

Aidha Mbali ya adhabu hiyo pia mahakama imetoa Amri ya kutaifisha meno hayo ya tembo na pikipiki moja yenye namba za usajili MC. 956 ATY aina ya GSM iliyokuwa inatumika kusafirisha nyara hizo.

Washtakiwa wote wawili wameshindwa kulipa faini hizo na kupelekwa gereza la wilaya ya Bukoba kutumikia vifungo vyao.