Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (aliyesimama kulia) akimkabidhi mkoba wenye nyaraka mbalimbali za Ofisi yake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) ndugu Isack Kihwili alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na viongozi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

………….. 

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Isack Kihwili, katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Dkt. Possi amezungumza na viongozi hao kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Bodi hiyo.
Aidha, Dkt. Possi amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa DIB mkoba wenye nyaraka mbalimbali za Ofisi yake, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) ndugu Isack Kihwili akizungumza na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisi kwake jijini Dar es Salaam.

 Viongozi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha viongozi hao kilichofanyika Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (aliyesimama kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), ndugu Isack Kihwili walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha viongozi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kilichofanyika Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.