************************************
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Stendi ya kisasa ya Daladala ya Mwenge inayojengwa kwa kiasi cha Shilingili Bilioni tano fedha zinazotokana na makusanyo ya ndani ya Manispaa hiyo.
Mhe. Chongolo ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara yake ikiwa ni muendelezo wa kukagua miradi inayojengwa na Manispaa pamoja na Serikali kuu na kusema kuwa hadi kufikia Oktoba mwaka huu standi hiyo itakuwa imekamilika na hivyo kutoa fursa kwa wafanyabiashara zaidi ya 600 kuendesha shughuli mbalimbali katika eneo hilo.
Ameongeza kuwa mradi huo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais John Pombe Magufuli na ilani ya uchaguzi iliyokuwa na lengo la kuwawekea wafanyabiashara wa kati na wadogo mazingira bora ya kufanya shughuli zao hivyo akawasihi Wananchi kutumia fursa hiyo.
“Serikali ya Rais Dk. Magufuli inawajali wafanyabishara wakubwa, wakati na wadogo, ndio mana Manispaa yetu ya Kinondoni kwakushirikiana na Serikali kuu hivi sasa inajenga Masoko ya kisasa, na hata kwenye hii stendi kutakuwa na maeneo kwa ajili ya kufanyashughuli za kibiashara jambo ambalo litaleta ufanisi mkubwa katika kuendeleza uchumi wetu wa kati” amesema Mhe. Chongolo.
Mradi huo wa ujenzi wa Standi ya kisasa Mwege unajengwa na Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ kwa mfumo wa Local Fundi ( Force Account) ulianza Aprili mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine utaiwezesha Manispaa kukusanya mapato na hivyo kuendeleza ukuaji wa uchumi wa kati.