Angel Di Maria (kushoto) akishangilia na Neymar baada ya kufunga bao moja na kutoa pasi mawili katika ushindi wa 3-0 wa Paris Saint-Germain dhidi ya Rasen Ballsport Leipzig ya Ujerumani kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa Luz Jijini Lisbon, Ureno. Di Maria alifunga bao la pili dakika ya 42 baada ya kumsetia Marquinhos kufunga la kwanza dakika ya 13 kabla ya kumpasia Juan Bernat kufunga la tatu dakika ya 56 na baada ya kuitoa RB Leipzig, sasa PSG itakutana na mshindi kati ya Olympique Lyon ya Ufaransa pia na Bayern Munich ya Ujerumani katika fainali Jumapili PICHA ZAIDI SOMA HAPA