Home Mchanganyiko DKT.ROBERT FYUMAGWA ATEULIWA KUWA KAIMU MKURUGENZI MKUU TAWIRI

DKT.ROBERT FYUMAGWA ATEULIWA KUWA KAIMU MKURUGENZI MKUU TAWIRI

0
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Wanyamapori Tanzania- TAWIRI Dkt Robert Fyumagwa (kulia). Kushoto  ni aliyekua Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Simon Mduma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori Tanzania- TAWIRI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Malasili na Utalii, Dkt.Aloyce K. Nzuki akizungumza jambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori – TAWIRI ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria, Dkt.Simon Mduma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akizungumza na Wajumbe wa  Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori katika Kikao kilichofanyika kwenye Ofisi za TAWIRI, Jijini Arusha.

………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki amemkabidhi majukumu rasmi Dkt. Robert Fyumagwa ya kuwa Kaimu  Mkurugenzi  Mkuu Taasisi ya Utafiti wa  Wanyamapori Tanzania- TAWIRI.

Dkt. Robert Fyumagwa anatekeleza majukumu ya Taasisi hiyo kufuatia aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori-TAWIRI, Dkt.Simon Mduma  kustaafu kwa  mujibu wa sheria.

Kupitia hatua hiyo Dkt.Fyumagwa ameanza rasmi kutekeleza majukumu ya Taasisi hiyo kuanzia tarehe 17 Agosti, 2020.

Akizungumza Jijini Arusha katika Kikao na Menejimenti ya TAWIRI,   Dkt. Nzuki amewataka  watumishi hao  kumpa ushirikiano Dkt. Fyumagwa  katika kutekeleza majukumu yake ikiwa pamoja na  kuimarisha  shughuli za utafiti wa Wanyamapori pamoja na kuendeleza  sekta ya wanyamapori nchini.