………………………………………………………
Watani wa jadi Tanzania Yanga na Simba mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu bara msimu wa 2020/21 unatarajiwa kuchezwa Oktoba 18 mwaka huu katika uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Almas Kasongo wakati akitangaza Ratiba ya Ligi hiyo iliyotoka Leo huku Mabingwa Simba wataanza ugenini dhidi ya wageni wa Ligi timu ya Ihefu FC mcheso utakaopigwa uwanja wa Sokoine Mbeya.
Mabingwa wa kihistoria nchini Yanga wao wataanzia nyumba kwa kuwakaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa moja kamili usiku.