Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari(hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Serikali ya Aawamu ya Tano katika Sekta ya Madini na Nishati, Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO, JNICC Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari(pichani), kuhusu mafanikio ya Serikali ya Aawamu ya Tano katika Sekta ya Madini na Nishati, Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO, JNICC Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari( hwapo pichani), kuhusu mafanikio ya Serikali ya Aawamu ya Tano katika Sekta ya Madini na Nishati, Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO, JNICC Jijini Dar es Salaam
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
***********************************
Na.Paschal Dotto-MAELEZO
Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza kwa kiasi kikubwa kwa kufanya mageuzi makubwa ambayo yemewezesha kulinda na kuwapa watanzania umiliki halali wa Rasilimali za Taifa ikiwemo madini ambayo kabla ya miaka mitano ya Serikali ya Rais Magufuli yalikuwa yanamanufaa machache kwa wananchi.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi amesema kuwa Mifumo ya Karne ya 21 ambayo Rais Magufuli ameiweka katika Sekta hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kulinda rasilimali hiyo ambayo ni adhimu kwa taifa na duniani kwa ujumla.
Dkt.Abbasi alieleza mifumo hiyo ni pamoja na kuimarisha mifumo ya kisheria na kitaasisi ambayo imewezesha sekta hiyo kuwa na usimamizi madhubuti na kuongeza uzalishaji na mapato kwa taifa kupitia madini.
“Tume ya Madini imeanza kazi kwa kasi katika kipindi hiki, marekebisho na kutungwa kwa sheria mpya za kusimamia mikataba yenye changamoto na umiliki wa madini vimefanyika na kuleta mageuzi makubwa nchini jambo ambalo ni utekelezaji mkubwa wa Serikali ya Aawmu ya Tano”, Amesema Dkt.Abbasi.
Alisema kuwa mifumo mingine ni pamoja na umiliki wa watanzania kwenye rasilimali hiyo ambapo baada ya kubadili mifumo na sheria katika sekta ya madini kampuni ya Twiga Minerals Corporation Limited ambayo iliundwa kufuatia maelewano kati ya wawekezaji, Barrick na Serikali imelete modeli mpya Afrika kwani watanzania wanaumiliki wa Migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.
Katika mabadiliko hayo sekta ya madini imeongeza kwa kiasi kikubwa katika unafuu wa wachimbaji wadogo na kusababisha kuongezeka kwa leseni katika maeneo ya uchimbaji hapa nchini.
“Ukiangalia idadi ya utoaji wa leseni kwa ajili ya uwekezaji mdogo, wa kati na mkubwa katika sekta ya madini. Idadi ya leseni zilizotolewa iliongezeka kutoka 3,484 hadi 7,32 kama inavyoainishwa, pia Serikali ilipunguza kodi kuwapa unafuu wawekezaji wadogo”, amefafanua Dkt.Abbasi.
Aidha, Katika kipindi cha Miaka mitano, Rais Magufuli aliagiza kuondolewa kodi zenye jumla ya asilimia 23 zilizokuwa zikikatwa kwa wachimbaji wadogo wanapouza madini yao (kodi ya zuio (withholding tax – 5% na kodi ya ongezeko la thamani VAT -18%)
Mfumo Mwingine ambao umewezesha kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa makusayo ni kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini ikiwa ni moja ya mafanikio ya Rais Magufuli katika sekta ya madini ambapo hadi Juni, 2020, jumla ya masoko ya madini 31 na vituo vya ununuzi wa madini 39 vilianzishwa maeneo mbalimbali nchini huku faida yake kubwa ikiwa ni kuongezeka kiwango cha madini yanayojulikana kuwa yamezalishwa na kuongezeka kwa mapato ya Serikali.
Dkt Abbasi alitolea mfano wa mchimbaji mdogo Saniniu Layzer ambaye Juni 24, 2020 aliishangaza dunia baada ya kuiuzia Serikali Madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 9.27 na kisha akapata jiwe la kilo 5.80 yenye jumla ya thamani ya TZS 7,744,152,703.82 na lile la Agosti 3, 2020 uzito wa kilo 6.3317 lenye thamani TZS 4,846,537,271.12, ni ushuhuda wa mafanikio ya Ukuta wa Mirerani ambao Rais Magufuli aliagizwa ujengwe na kuwekewa camera za ulinzi ili kuepusha utoroshaji wa madini hayo adimu duniani.
Ujenzi na usimamizi bora wa Ukuta katika mgodi wa madini ya Tanzanite Mererani Mkoani Arusha umeiwezesha Tanzania kuingia kwenye historia kupatikana kwa madini ya tanzanite yenye uzito na thamani hiyo kubwa ambayo yaliiwezesha Serikali kupitia Tume ya Madini kukusanya maduhuli ya Shilingi 881,348,298.25.
Katika Kipindi cha Miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano imewezesha kuongezeka kwa ukusanyaji maduhuli ambapo Serikali iliwekea malengo ya kukusanya bilioni 470 kuanzia mwaka 2015/16 hadi 2019/20 ambapo Serikali imeweza tumevunja rekodi kwa kukusanya TZS Bilioni 528 mwaka wa Fedha 2019/20.