Home Mchanganyiko Mageuzi Makubwa ya JPM, Sekta ya Nishati yamewatoa wananchi Gizani.

Mageuzi Makubwa ya JPM, Sekta ya Nishati yamewatoa wananchi Gizani.

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya  Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari( hwapo pichani), kuhusu mafanikio ya Serikali  ya Aawamu ya Tano katika Sekta ya Madini na Nishati, Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO, JNICC Jijini Dar es Salaam

Picha na Idara ya Habari-MAELEZO

************************************

Na Paschal Dotto-MAELEZO.

15 Agosti 2020.

Serikali Imetekeleza ujenzi wa Miundombinu ya uzalishaji Nishati ya Umeme ambapo kufikia sasa miradi iliyojengwa imewezesha kuimarisha upatikanani wa nishati hiyo kwa wananchi na kuwawezesha kupata huduma muhimu katika maeneo yao.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi amesema kuwa mpaka sasa Serikali imeweza kutekeleza miradi mikubwa ambayo na  kuondoa adha ya upatikanaji wa umeme nchini.

“Serikali ya Dkt. Magufuli pia imetumia takribani TZS Trilioni 1.109 ya fedha za ndani kutekeleza miradi mikubwa miwili ya umeme wa gesi,  Kinyerezi-I Extension megawati 185 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 188 sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 315.4; na Kinyerezi II MW 248.22 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 344 sawa na Shilingi bilioni 794.12”, Amesema Dkt.Abbasi.

Dkt. Abbasi alisema kuwa Katika kipindi cha 2015-2020 mafanikio yafuatayo yamepatikana katika sekta ya Nishati ikiwemo ongezeko la uzalishaji umeme wa miradi miwili ya kinyerezi ambayo inahusisha gesi na kufikia Disemba mwaka huu jumla ya megawati 583.22 za umeme wa gesi zitaingizwa kwenye Gridi ya Taifa (Kinyerezi I, Kinyerezi I Etension na K-II.

Alieleza kuwa ongezeko hilo la umeme limewezesha kuondokana na mgawo wa umeme kwani hadi kufikia Julai 2020, jumla ya megawati 1,602.32 zimeongezeka  kutoka megawati 1,308 mwaka 2015, na hiyo imesaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Pia alieleza namna TANESCO ilivyojiimarisha na kuwezesha mikoa mingi kuingia kwenye gridi ya taifa ikiwemo mikoa ya Lindi, Njombe na Ruvuma na kusaidia kuachana na matumizi ya mitamboa ambayo yalikuwa yanasababisha gharama kubwa kwa shirika hilo

“Kwa mara ya kwanza tangu Uhuru, mikoa ya Lindi, Mtwara, Njombe na Ruvuma imeingia katika Gridi ya Taifa na kusaidia kuachana na  kutumia mitambo ya mafuta mazito ambayo ilikuwa inaigharimu TANESCO wastani wa Shilingi bilioni 15.3 kwa mwaka katika mikoa hiyo, lakini pamoja na mitambo ya mikoani kuzimwa, TANESCO pia iliachana na kununua umeme kutoka mitambo binafsi ya mafuta mazito na kuliwezesha Shirika kuokoa matumizi ya Shilingi bilioni 118.175”, Alisema  Dkt.Abbasi.

Akizungumzia Sekta ya gesi asilia, Dkt.Abbasi alieleza kuwa Serikali kupitia TPDC imeendelea kusambaza gesi asilia kwa wateja wa majumbani na viwandani katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara na Lindi, adi kufikia, Juni, 2020, zaidi ya nyumba zipatazo 500 na viwanda zaidi ya 48 vimeunganishwa. Aidha, zaidi ya magari 400 yamefungwa mifumo ya matumizi ya gesi asilia ikilinganishwa na magari 60 yaliyokuwa yameunganishwa mwaka 2015.

Pia, Serikali ya Awamu ya Tano, imeendelea na Mpango Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini: Hadi Julai, 2020 jumla ya vijiji 9,412 vimeunganishwa kutoka vijijini 2,018 mwaka 2015, ikiwa ni sawa na ongezeko la vijiji 7,394, Jumla ya Shilingi trilioni 2.29 zimetumika ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 1.78 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 515.71 ni fedha za nje kutoka kwa Washirika wa Maendeleo

Aliongeza kuwa katika Miaka mitano  20215-2020 Serikali imeanza utekelezaji wa Mradi Mkubwa wa kihistioria  wa Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) MW 2,115 na hadi sasa Serikali imeshatoa TZS. Trilioni 1.38 kati ya Trilioni 6.5 na mradi unaendelea kutekelezwa katika hatua mbalimbali zikiwemo Uchorongaji wa handaki la kuchepusha maji (Diversion Tunnel) wenye kimo cha mita 19, upana wa mita 14 na urefu wa mita 703 umekamilika. 

Hatua nyingine ambayo imefikia katika Mradi huo mkubwa kwa Afrika Mashariki na Ukanda wa SADC na wanne kwa ukubwa barani Afrika katika kuzalisha umeme ni Ujenzi wa kingo na msingi (foundation excavation and treatment) wa Tuta Kuu (Main Dam) la kuzuia maji lenye urefu wa mita 1,025 na kimo cha mita 131 ili kutengeneza bwawa unaendelea. Sehemu hii ya kazi imefikia wastani wa asilimia 65; Ujenzi wa kingo na msingi unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba 2020 kulingana na mpango kazi wake.

Zingine ni Uchorongaji wa sehemu ya kuanzia mahandaki ya kupeleka maji kwenye mitambo ya kuzalisha umeme (Power Intake) unaendelea ambapo na hatua iliyofikiwa ni  asilimia 88,  Kwa sasa kazi zinazoendelea zinahusiana na uchorongaji wa mahandaki matatu (Power Tunnels) ya kupeleka maji mgodini kama ifuatavyo, Handaki namba 1 lenye urefu wa mita 470, Maandalizi kwa ajili ya uchorongaji yamekamilika, Handaki namba 2 urefu wa  mita 410, Maandalizi kwa ajili ya uchorongaji yamekamilika Handaki namba 3 urefu wa mita 350 uchorongaji unaendelea ili kukamilisha mradi huo wenye kuzalisha Megawatt 2,115.