NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba imefanikiwa kupata saini ya Kiungo wa Kimataifa wa Powere Dynamos ya Zambia Larry Bwalya ambaye alikaribia kidogo kutua kwa mahasimu wao Yanga.
Nyota huyo ametua leo Bongo kwa ndege ya shirika la Ethiopia Airlines na kumalizana na Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania.
Nyota huyo ana uwezo wa kutumia mguu wa kushoto anaungana na kiungo mwenzake mnyumbulifu Clatous Chama, mwamba wa Lusaka ambaye naye anatokea pia Zambia.