Home Mchanganyiko UTPC yawawezesha Waandishi wa Habari Manyara juu ya magonjwa ya Mlipuko.

UTPC yawawezesha Waandishi wa Habari Manyara juu ya magonjwa ya Mlipuko.

0

**********************************

Na John Walter-Manyara

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Manyara (MNRPC) kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) wameendesha mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari ambao ni wanachama wa klabu hiyo juu ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo COVID-19 na namna ya kujilinda, kufanya kazi na kujikinga kwenye magonjwa hayo. 

Mafunzo hayo yamefanyika leo Agosti 15, 2020 katika ukumbi wa Giraffe katika hotel ya White rose mjini Babati yakiwezeshwa na wataalam wa afya kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoani humo.

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya ya Babati  Lazaro Twange  ametoa wito  kwa waandishi wa habari kuzingatia weledi katika Kazi zao pindi wanaporipoti matukio ya magonjwa ya mlipuko ili kuondoa taharuki kwa wananchi.

Amesema mafunzo hayo  yaliyotolewa yanagusa sehemu kubwa ya jamii na njia zake za uenezaji ni rahisi kuzuilika kupitia elimu itakayotolewa kupitia vyombo vya habari.