********************************
Na Masanja Mabula, Pemba.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linamshikilia kijana Abdi Azan Hamad 18 mkaazi wa wilaya ya Wete, anayetuhumiwa kuwadhalilisha watoto wawili wa kiume.
Watoto hao wa familia mmoja ana umri wa miaka 8 na mwengine miaka 7 walifanyiwa kitendo hicho wakati wakiwa katika bonde la Mpunga la Sharif wakiinga ndege.
Akithibitisha kutokea tukio hilo ,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kamisha Msaidizi Mwandamizi , Juma Sadi Khamis alisema tukio hilo limetokea 10/08/2020 saa sita mchana.
Kamanda Sadi alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo alifika katika bonde hilo na kuwafanyia watoto wao kitendo cha udhalilishaji ambapo waliporejea nyumba walitoa taarifa kwa wazazi wao.
“Kwa sasa tunamshikilia kijana Abdi Azan Hamad huyu anatuhumiwa kuwaingilia watoto wawili wa kiume mmoja akiwa na miaka 8 na mwengine miaka 7, upelelezi ukikamilika tutamfikisha mahakamani”alisema Kamanda.
Aidha Kamanda Sadi aliwataka wazazi kuwa karibu zaidi na watoto wao ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi ya simu ili kuwajenga kuwa maadili mema.
“Jeshi la Polisi limepokea ripoti ya daktari aliyewafanyia uchunguzi watoto hao, ambayo imethibitisha kwamba kitendo hicho walifanyiwa.
Naye sheha wa Shehia husika Omar Mussa(sio jina lake sahihi) alisema jamii inasumbuliwa rusha muhali hali ambayo inakwamisha watuhumiwa na matendo kushindwa kutiwa hatiani.
Alisema iwapo jamii itakuwa tayari kushirikiana na vyombo vya sheria , wahusika wapatiwa hatiani na hivyo kuwa fundisho kwa wenye tabia ya kudhalilisha watoto na wanawake.