Home Uncategorized RC KUNENGE AMUAPISHA MKUU MPYA WA WILAYA YA ILALA.

RC KUNENGE AMUAPISHA MKUU MPYA WA WILAYA YA ILALA.

0

**********************************

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amemuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija alieteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza Wilaya hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo RC Kunenge amewaelekeza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia ipasavyo suala zima la ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za serikali pamoja na kusimamia suala la Mazingira.

Aidha RC Kunenge amewataka wahakikishe wanaboresha mazingira ya uwekezaji huku akiwataka watumishi wa Mkoa huo kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu ili kwa pamoja watatue kero za wananchi.

RC Kunenge pia amewahimiza Wakuu wa Wilaya kusimamia suala la Ulinzi, Usalama na Amani hususani kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija ameeleza kuwa ataenda kusimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi wa Wilaya hiyo.