Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Lindi wakati wa ziara yake mkoani hapo ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) pamoja na kuzungumza na wadau wa sekta anazozisimamia mnamo Agosti 11,2020.Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Bibi.Rehema Madenge.
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bibi.Rehema Madenge akitoa taarifa fupi ya Mkoa kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe , kuhusu sekta anazozisimamia wakati wa ziara ya Waziri huyo mkoani hapo ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) pamoja na kuzungumza na wadau wa sekta anazozisimamia mnamo Agosti 11,2020.
Mhandisi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi.Upendo Mbelle akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ya kukagua usikivu wa shirika hilo pamoja na kuzungumza na wadau wa sekta anazozisimamia mkoani Lindi mnamo
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Mkoa wa Lindi na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati wa ziara yake mkoani hapo ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) pamoja na kuzungumza na wadau wa sekta anazozisimamia mnamo
Mhandisi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi.Upendo Mbelle (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) wakati wa ziara ya kukagua usikivu wa shirika hilo mkoani Lindi pamoja na kuzungumza na wadau wa sekta anazozisimamia
Fundi Mitambo wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw.Hamis Kalanje akimuonyesha mitambo ya kurushia matangazo ya redio iliyopo Kihipe mkoani Lindi Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto),wakati alipotembelea kituo hicho
……………………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki –WHUSM,Lindi.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amesema kwamba suala la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika mikoa ya Lindi na Mtwara linasababisha mitambo ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kushindwa kufanya kazi ipasavyo, hivyo suala hilo linapaswa kushugulikiwa haraka.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo Agosti 11, 2020 alipokua katika ziara ya kukagua mitambo ya TBC iliyopo Kipihe mkoani Lindi ambapo amesema suala hilo ni la kisera hivyo ataliwasilisha Wizara ya Nishati ili litafutiwe ufumbuzi wa kudumu.
“Maeneo ya kimkakati hayapaswi kukosa umeme wa uhakika,Eneo hili la Kipihe ni mojawapo ya maeneo ya kimakati ambayo yanasaidia shirika letu la utangazaji TBC,kutoa habari kwa wananchi wa mikoa ya kusini hivyo umeme lazima uwe wa uhakika utakaowezesha mitambo hiyo kufanya kazi kwa ufanisi na muda wote”alisema ,Mhe.Mwakyembe.
Mhe.Mwakyembe ameongeza kuwa TBC,ni chombo cha umma ambacho kina wajibu wa kuelezea wananchi nini Serikali imefanya katika nchi na inatarajia kufanya nini katika siku zijazo hivyo changamoto yoyote inayojitokeza katika chombo hicho ni lazima itafutiwe ufumbuzi wa haraka.
Kwa upande wake Mhandisi wa Shirika hilo Bibi.Upendo Mbele amesema kwamba usikivu wa shirika hilo umeendelea kuimarika ambapo maeneo mengi yanafikiwa kwa ubora unaotakiwa kufuatiwa kufungwa mitambo ya kisasa katika mkoa huo.
Bibi.Upendo ameongeza kuwa ndani ya wiki mbili zijazo eneo la Kipihe litawekewa jenereta ambalo litasaidia pale umeme unapokatika mitambo isizimike ambayo inasababisha matangazo ya redio kukatika,huku akieleza kuwa Mwaka wa fedha 2020/2021 TBC imetenga fedha kwa ajili ya kuimarisha studio ya Kanda ya Kati Dodoma.
…MWISHOO..