Home Michezo JESHI LA AKIBA LANOLEWA MIHAMBWE

JESHI LA AKIBA LANOLEWA MIHAMBWE

0

…………………………………………………………………………….

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Mwenyekiti Kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amefanya ziara ya siku moja kijiji cha Mpunda kata ya Michenjele kuwatembelea Wanafunzi wanaopewa mafunzo ya Jeshi la Akiba kwa Tarafa ya Mihambwe.

Gavana Shilatu amewaambia Wanafunzi hao kuzingatia nidhamu, uadilifu na uzalendo kwa Taifa kwani ndio siri ya mafanikio kwa kila jambo.

“Mkitanguliza nidhamu, uadilifu na uzalendo kwa Taifa letu la Tanzania ndio misingi mikuu ya mafanikio. Tunatarajia mafunzo haya kufunguliwa wiki hii ikiwa ni miaka 15 imepita tangu kufanyika kwa mafunzo haya mara ya mwisho.” Alisema Gavana Shilatu.

Wanafunzi toka katika vijiji na vitongoji vya Tarafa ya Mihambwe wamejitokeza kwa hiari yao kupewa mafunzo ya Jeshi la akiba ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya Tarafa ya Mihambwe na viunga vyake.