Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akiwasilisha tarifa yake katika Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu akichangia katika Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (Kwanza Kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu akiendesha kikao hicho na katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Miriamu Mbaga na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo (kushoto). Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akichangia katika Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu na wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (Kwanza Kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu akiendesha kikao hicho na Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Miriamu Mbaga. Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriamu Mbaga akifungua Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima(katikati) akifrahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Mkurugenzi wa Kinga Wzara ya Afya, Dkt. Leonard Subi (kulia) wakati Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akionyesha vifaa vitendanishi kwa wajumbe wa Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Afya wa Mkoa wa Simiyu wakifatilia mjadala unaoendelea katika Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu.
………………………………………………………….
Na.Majid Abdulkarim, Simiyu
Serikali imeaagiza mikoa yote nchini kufanya ukaguzi mara moja katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi ili kujua kitu gani kinaendelea kwenye mfumo na mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba ,vitendanishi na kuchukua hatua stahiki zikiwemo za kuziba mianya hiyo mara moja.
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima katika Kikao kazi cha tathmini ya taarifa ya utekelezaji wa ukaguzi wa mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na mapato ya uchangiaji katika vituo vya kutolea huduma za afya Mkoani Simiyu.
Aidha Dkt. Gwajima ameeleza kuwa kuna baadhi ya watu nchini wamegeuza Serikali kuwa shamba la bibi kwamba kila mtu atafanya anavyojisikia huku watanzania wanyonge wanataabika.
“Hivyo uchunguzi huo ufanyike ndani ya miezi mitatu na kuleta taarifa ifikapo 15 Oktoba, 2020 ili kujua nini kinaendelea katika vituo vyetu, hatua gani zimechukuliwa ngazi ya Halmashauri na Mkoa na zipi zichukuliwe ngazi ya kitaifa kulingana na matokeo ya zoezi hilo”, ameelekeza Dkt. Gwajima.
Dkt. Gwajima amesema kuwa, sharti ukaguzi huo ufanywe na wataalamu wa ukaguzi na uchunguzi yaani wakaguzi wa ndani (CIA) mkoa, halmashauri na maafisa ugani wa ngazi husika kama ilivyofanyika hapa Simiyu .
Kwa kuongezea Dkt. Gwajima amesema kuwa mikoa mingine iliyotii na kutekeleza maelekezo ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na kubaini hayo waliyobaini ambayo hayakubaliki kamwe kuendelea kutokea katika vituo hivyo.
Dkt. Gajima amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kutoa ushirikiano wote stahiki kwa timu hizi za ukaguzi ili kuweza kukamilisha zoezi hilo ka ukamilifu.
“Hivyo, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri muwawezeshe Wataalamu , Wakaguzi hawa na Wale Wakuu wa Mikoa na Wilaya mtusaidie kufuatilia utekelezaji kama ambavyo Mhe Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alivyokuwa mstari wa mbele kushirikiana na Katibu Tawala wake na sasa wameona matunda kuwa kumbe inawezekana dawa, vifaa tiba na huduma za vipimo kuwepo na vituo vikaongeza mapato ya uchangiaji hadi zaidi ya mara 4 ndani ya miezi sita tu, Simiyu wamethubutu, wameweza na wameiona tija hivyo wengine chukueni hatua kwa kujifunza toka kwao”, amesema Dkt Gwajima.
Pia Dkt. Gwajima amebainisha kuwa katika fedha na mali yoyote ya Serikali hakuna mchezo wa mzaha hivyo kila mtumishi mwenye dhamana ya kusimamia anao wajibu wa kutoa taarifa ya matumizi.
Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima amesema kuwa ni lazima yapatikane mapinduzi makubwa na ya haraka katika kutunza raslimali za afya kwani haiwezekani Serikali itupe mtaji mkubwa wa raslimali dawa, vifaa tiba na vitendanishi, mishahara, majengo, ilipe umeme na maji halafu turudi tena kusubiri itugawie hela zingine kila mwezi na takwimu za ukaguzi wa awali hapa Simiyu zinakiri kuwa inawezekana kupunguza utegemezi.
Dkt Gwajima amesema kuwa mikoa mingine iliyofanya vizuri kwenye ukaguzi huo kuwa ni Morogoro, Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Arusha.
“tafadhali nawaagiza ukaguzi huo uwe endelevu na usiwe ukaguzi wa macho bali wa vitendo kwa takwimu sahihi zenye ukweli ili wachezea mali ya umma wauone ukweli kwa macho na masikio yao kuwa hatuna mchezo na hatuonei mtu ni kweli mtupu na wao ni mashahidi”, ameagiza Dkt. Gwajima.
Dkt. Gwajima amelekeza kuwa lazima kila mkoa na halmashauri uhakikishe vituo vyote vina vitendea kazi vya utunzaji mali ya umma vikiwemo leja za mali, vitabu vya kuombea na kutolea mali toka stoo (requisition and issue vouchers), kadi za kufuatilia rekodi za mali inayotoka (bin cards), risiti za dawa (prescriptions), fomu namba 2C ya mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) na watumiaji wa vifaa hivyo wanafundishwa na kuelewa na kumiliki na kutumia na kufanyiwa ufuatiliaji wa utumiaji.
Lakini pia Dkt. Gwajima amesema ipo mifumo mbalimbali ya kiteknolojia (TEHAMA) ambayo inatunza kumbukumbu za raslimali za afya mfano ELMIS lakini ajabu ni kuwa Wakaguzi wa Ndani na Maafisa Ugani hawajawezeshwa kuifahamu na kupewa Nywila (Password) ili wawe huru kuingia na kufuatilia ikiwemo kukagua .
Hivyo ameagiza wawezeshwe na wapewe Nywila na Uhuru kamili wa kuingia katika mifumo hiyo na kufanya kazi yao ya ukaguzi maana hakuna sababu wala maelezo kwa nini waliachwa wakati mfumo huo unawahusu.
Dkt. Gwajima ametoa wito kufungwa mfumo wa GOTHOMIS maana sababu za kutofunga ni nyepesi mno kila kituo kiano uwezo ila tatizo vinatafutwa sababu zisizo kuwa na msingi kuwa hakuna hela huku usimamizi wa makusanyo uko legelege na imeonekana wazi mapato yakisimamiwa yanaongezeka hadi zaidi ya mara 4 hivyo mfumo huo ufungwe na kila mwezi kuwe na taarifa ya hatua zilizoendelea na asiyefunga anahitaji kufanyiwa ukaguzi maalumu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Miriam Mbaga kuunda kikosi kazi kitakacho fanya uchunguzi juu ya upotevu wa dawa katika halmashauri zote katika mkoa huo na kuja na taarifa ya kitakacho patikana.
“Taarifa ikionesha kuwa umekula fedha ya Serikali, umesababisha fedha au mali kupotea kwa uzembe sisi kama watumishi, watendaji na wasaidizi wa Mhe. Rais Magufuli hatutakuwa na lingine zaidi ya kuchukua hatua za kuhakikisha kwanza mtumishi huyo anarudisha fedha hizo na hatua ya pili anafikishwa kwenye vyombo stahiki vya dola ili hatua zaidi za kisheria zifuate”, ameeleza Mtaka.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mbaga amesema kuwa amepokea maelekezo hivyo kuanzia kesho atakaa na Wakurungenzi wote na Watendaji wake kuweka mipango mikakati ya kutekeleza maagizo hayo kwa wakati ili kuokoa upotevu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili juhudi za Serikali ziendelee kugusa wanachi wenye uhitaji kama ilivyokusudiwa.
“Mimi nafikika wakati wote na watu ambao wana asili ya kuwajibika kwa kutoa matokeo chanya kwa wakati watanipata muda wote ila wazembe, wasio na matokeo kila siku Mkuu Mkuu matokeo hakuna hao hapana hatutaelewana kwani sote lengo ni kuleta matokeo chanya katika mkoa wetu “, amesisitiza Bi. Mbaga