Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wakati alipotembelea Maonesho ya 27 ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi katika Viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi katika Viwanja vya Themi Mara baada ya kujionea Nyavu ambazo wanatumia katika Kuvulia samaki katika Bwawa la Nyumba ya Mungu.
Naibu waziri Abdallah Ulega akisikiliza kwa makini maelekezo ya Mkulima wa mbegu za Kabeji Katika maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
*********************************
Na.Mwandishi Wetu-Arusha.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaagiza Viongozi wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuhakikisha kuwa wananunua Viatu kutoka kiwanda Cha Kilimanjaro Leather Industries Co. ltd ,kilichopo Moshi katika Gereza la Karanga Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na wananchi wa Kanda ya Kaskazini katika Viwanja vya Themi Njiro Nane Nane,Ulega alisema kuwa ni lazima viongozi wa mikoa hiyo wawe mfano wa kuweza kuratibu na kununua viatu katika kiwanda hicho.
Alisema kuwa kiwanda hicho kimejengwa na Serikali kwa shilingi bilioni 69,ambao Raisi dkt.John Pombe Magufuli alitoa fedha hizo ili kuhakikisha
Kiwanda hicho Cha kuchakata ngozi na kuzalisha bidhaa nyingine Mbali Mbali za ngozi kinajengwa hapa nchini.
Aidha Ulega alisema kuwa kwa kuwa kiwanda cha Karanga kitakuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha Viatu Hadi kufikia jozi milioni 1.5 kwa Mwaka,hivyo Watanzania kutumia bidhaa hizo haswa Viatu.
“Nawataka ninyi viongozi mliopo hapa wa mikoa hii ambao mmesifiwa Sana hapa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta kuwa mpo vizuri,ratibuni hakikisheni kuwa msimu wa January mwakani watoto wetu wa mikoa hii wanavaa Viatu vya kiwanda hiki,kwanza vina ubora,bei zake ni nafuu na ni bidhaa kutoka kwetu,muone fahari ndugu zangu Watanzania mfano huu uanzie Sasa hapa Kaskazini.”alisema
Ulega.
Alitoa Rai kwa viongozi kulinda viwanda vya ndani kwa kuhakikisha kuwa wanavitembelea mara kwa mara,kuvitizama na kuangalia changamoto zilizopo na kuzitatua ili vifanye uzalishaji wao vizuri.
“Hakikisheni kuwa kazi hii mnanifanya wenyewe msisubirie waje watu kutoka nje ili waweze kuwafanyia Mambo yenu,tuvilinde tulivyonavyo ili viweze kutusaidia na kutusitiri,pamoja na kukuza Uchumi wetu.”alisema Ulega.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti aliwataka wakulima,wafugaji na wavuvi kuhakikisha kuwa wanatumia maonesho hayo kuweza kutambua mchango wa taasisi Mbali Mbali za fedha ili wazitumie kukuza shughuli zao.
“Taasisi hizi za fedha zimekuwa Ni changamoto kwa Makundi haya Sasa tumezileta hapa ili wakulima,wafugaji,na wavuvi waweze kufanya vyema na kukuza Uchumi wao.”alisema Mkirikiti
Maonesho ya 27 ya Kilimo na Mifugo na Uvuvi yanahitimishwa leo August 10 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema kuwa”Kwa Maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020.”