……………………………………………………..
Na Calvin Gwabara, Morogoro
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Mhe. Umma Mwalimu Amelia huku tu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Wataalamu wake kwa msaada Mkubwa waliotoa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa COVID 19.
Mhe. Mwalimu ameyasema hayo alipotembelea Banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwenye maonesho ya Wakulima nanenane Kanda ya Mashariki yanayofanyika Mkoani Morogoro kabla ya kufunga rasmi maonesho hayo Kikanda.
“Nitumie nafasi hii kuushukuru Uongozi mzima wa SUA na Watafiti wake kwa msaada Mkubwa mliotoa wakati wa mapambano ya COVID 19 Kwa kusaidia kwenye upimaji wa sampuli mbalimbali za wagonjwa kwa ubora mkubwa, Hakika Tina kila sababu ya kuwashukuru kwa jitihada hizi kubwa mlizozifanya” Alisisitiza Mhe. Umma Mwalimu.
Aliongeza “Wakati tunahangaika na zoezi la upimaji wa sampuli zilizokuwa zinakuja kwenye Maabara kuu kutoka nchi nzima mlitusaidia sana kupunguza mzigo wa upimaji sampuli zile baada ya nyinyi pia kuthibitika kuwa mnaweza kufanya kazi hii katika viwango vinavyokubalika”.
Waziri huyo wa Afya ametembelea mabanda mbalimbali ya maonesho na kujionea teknolojia na mbinu mbalimbali za Kilimo,Mifugo na Uvuvi kabla ya kufunga rasmi maonesho hayo ya Wakulima nanenane Kanda ya Mashariki.
Akiwa kwenye banda la SUA alijionea vifaa mbalimbali vya maabara na wataalamu ambao walishiriki kwenye zoezi hilo na Upimaji wa sampuli za washukiwa na Ugonjwa wa COVID 19 sambamba na Hospitali pekee Taifa ya Rufaa ya wanyama iliyopo chuoni hapo.
Waziri huyo wa Afya pia amepata nafasi ya kujionea Wataalamu na wajasiliamali wa masuala ya Lishe kutoka SUA ambao wanazalisha bidhaa mbalimbali kutokana na mazao lishe na kuwataka kuanza kufungasha bidhaa zao kwaajili ya wanunuzi wadogo kwa bei nafuu ili hata watoto waweze kununua kwa hela ndogo.
Maonesho hayo ya Wakulima nanenane yafanyika kwenye Kanda mbalimbali na yalianza tarehe 1/8/2020 na kufikia kilele tarehe 8/8/2020 lakini Serikali imeongeza siku mbili ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kujifunza na pia waonyeshaji kufanya biashara zao.
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kama Mdau Mkubwa wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi kimeshiriki kwenye maonesho hayo Kitaifa Mkoani Simiyu na Kikanda kwenye Kanda ya Mashariki Mkoani Morogogoro.
Maonesho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Kwa Maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi chagua viongozi Bora Mwaka 2020”