Home Mchanganyiko TBL PLC ILIVYOSHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE 2020 MKOANI SIMIYU

TBL PLC ILIVYOSHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE 2020 MKOANI SIMIYU

0

 

Mtaalam wa upishi wa bia kutoka kiwanda  cha TBL tawi la Mwanza Mark Masolwa, akimkabidhi fulana mkazi wa lamadi, Guke Hamis baada ya kujibu maswali yaliyohusu unywaji wa kistaarabu,kwenye maonesho ya nanenane  katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Mtaalam wa upishi wa bia wa  kiwanda cha bia cha TBL tawi la Mwanza Mark Masolwa, akiwaeleza wananchi namna ya kunywa kistaarabu na mazao yanayotumika kupikia bia, kwenye maonesho ya nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu

Wananchi wa simiyu wakiangalia bidhaa za kampuni ya TBL walipotembelea banda lake.

Wananchi wa Simiyu wakiburudika na chapa za vinywaji vinavyotengenezwa na TBL kwenye uwanja wa maonyesho ya Nanenane

…………………………………………………..

Kampuni ya bia  TBL Plc, imeshiriki maonyesho  ya kuadhimisha Siku ya wakulima ya Nane Nane ambayo ilifanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakibindi mkoani Simiyu.

Wananchi wengi walitembelea banda lake la maonyesho na kupata fursa ya kuona bidhaa zake, kupata elimu ya unywaji wa kistaarabu pia kupata maelezo ya fursa za kilimo cha mazao ambayo kampuni inanua kwa ajili ya malighafi.