Home Mchanganyiko WAKULIMA WAMETAKIWA KTUMIA TAFITI ZA WATAALAMU WAZAWA

WAKULIMA WAMETAKIWA KTUMIA TAFITI ZA WATAALAMU WAZAWA

0


……………………………………………………………………….
NA FARIDA SAIDY,SIMIYU.
Wakulima Nchini wametakiwa kutumia Tafiti zinazofanywa na Wataalamu Wazawa ili kuleta matokeo chanya katika kukuza Sekta ya Kilimo na kuleta maendeleo katika kuzalisha mazao hali itakayopelekea kuongeza kipato chao na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Akiwa katika Banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) Profesa Raphael Chibunda ametoa wito huo, huku akiwataka Watanzania kuthamini kazi zinazofanywa na Wataalamu wazawa ambao unauwezo wa kujua mahitaji halisi ya wakulima.
Aidha, ameongeza kuwa wamekuja na Teknolojia mpya ya kufukuza wadudu waharibifu shambani kwa kutumia Ndege aina ya Bundi ambaye anakula Panya na wadudu wengine wasumbufu wa Mazao na kumfanya mkulima kutokutumia viuatilifu katika kufukuza wadudu hao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dr. Amos Nungu amesema COSTECH imewezesha watafiti mbalimbali katika kufanya Tafiti na kutoa matokeo kwa wananchi yalioyoleta manufaa na kuongeza uzalishaji wa Mazao Mbalimbali.
Vilevile, amesema wapo katika maonesho ya wakulima nanenane kwa lengo la kukutana na wadau wa Kilimo,Watafiti na Wabunifu ambao amewafadhili na kuhakikisha wakulima wanapata mbolea,dawa na Mbegu bora ambazo zinasaidia kupata mazao kwa wingi.
Hata hivyo amezitaka Halmashauli za Kanda ya Ziwa Mashariki kutumia fulsa ya maonesho ya wakulima nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi kwa kufika katika Banda la COSTECH ili kuweza kujua sifa mbalimbali za kushiriki katika mashindano ya Kitaifa ya Sayansi na Ubinifu (MAKISATU)
Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Sua Dr Philbet Nyinonde amesema chuo kimeanzisha kitengo maalumu kitakacho msaidia mkulima kupata taarifa zote muhimu kutoka kwa wataalam Kupitia simu yake ya mkononi.