Home Michezo DODOMA FC YATEMA 12 WALIOPANDISHA TIMU LIGI KUU, YASAJILI WATATU WAPYA

DODOMA FC YATEMA 12 WALIOPANDISHA TIMU LIGI KUU, YASAJILI WATATU WAPYA

0

BAADA ya kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao, klabu ya Dodoma Jiji FC imewaacha wachezaji 12 na kusajili wapya watatu hadi sasa.
Taarifa ya Dodoma FC imewataja wachezaji wapya waliosajiliwa ni Yussuf Abdul, Joseph Mapembe, Hamad Kibopile, Rajab Kibera, Joshua Soka, Aziz Gilla, Moka Shaaban, James Mendy, Ismail Makorosa, Moshi Mrisho, Mohamed Kilua na Ramadhan Mohamed ambaye amerejeshwa Azam FC baada ya kumaliza muda wake wa kucheza kwa mkopo.  
Walioongezewa mikataba ni Emmanuel Mseja, Hussein Masalanga, Anderson Solomon, Hassan Kapona, Mbwana Kibacha, Rajab Seif, Steven Mganga, Jamal Mtegeta, Deusdedit Kigawa, Santos Thomas na Khamis Mcha.

Wapya waliosajiliwa hadi sasa ni Michael Chinedu kutoka Alliance FC ya Mwanza, Seif Karihe kutoka Lipuli FC ya Iringa na Cleophace Mkandala kutoka Tanzania Prisons ya Mbeya.