Home Biashara WAKULIMA WAMETAKIWA KUJIKITA KATIKA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

WAKULIMA WAMETAKIWA KUJIKITA KATIKA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

0

Mkurugenzi wa Datta Drip Irrigation Bwana Yudas Luganza akitoa maelezo kwa wakulima wa Mbogamboga waliofika katika Maonyesho ya sikukuu za walikuma katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu

Wananchi mbalimbali waliofika katika Banda hilo
…………………………………………………………………………………….

NA FARIDA SAID, SIMIYU.

Kutokana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi wakulima Nchini wametakiwa kutumia teknolojia mbalimbali za umwagiliaji zinazotolewa na wadau ili waweze kulima na kuzalisha mazao kwa wakati ILI kuendana na kasi ya soko la ulimwengu.
Rai hiyo imetolewa na kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji Bwana Daudi Nicodemas akiwa katika Banda la Datta Drip Irrigation Africa (DATTADRIP) katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu katika sikukuu za wakulima Nanenane ambapo amesema kuwa wakulima wakibadilika kutoka kwenye kilimo cha kutegemea mvua za msimu hali ya chakulia itaimarika zaidi nchini.
Aidha, ameongeza kuwa katika kipindi hiki ambacho Taifa limeingia katika uchumi wa kati ni vyema wakulima wakaongeza uzalishaji wa mazao kwa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Datta Drip Irrigation Bwana Yudas Luganza amesema wao kama wadau wanashirikiana na tume ya umwagiliaji katika kuhakikisha wakulima wanapata elimu na vifaa vya umwagiliaji vitakavyowasaidia katika kilimo cha kisasa.
Aidha,amesema pamoja na kutoa elimu kwa wakulima lakini pia wanawasaidia wakulima kujenga vitalu nyumba pamoja na kusambaza vifaa vya umwagiliaji ambavyo vitamsaidia mkulima katika kilimo cha umwagiliaji.
Nao wananchi waliofika katika banda hilo akiwemo bwana Josephy Shima Pamoja na Bi. Mwashira shija wamesema wamejifunza vitu ambavyo vitawasaidia kutoka katika kilimo cha msimu na kujikita katika kilimo cha umwagiliaji.