Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani(katikati) Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(kulia) Katibu Mkuu Mhandisi Zena Said(kushoto) wakiwa kwenye kikao pamoja na wawekazaji wadogo wa umeme wa umeme nchini kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati,Mkoani Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Leonard Masanja(kushoto) Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Umeme Mhandisi Styden Rwebangila wakiwa kwenye kikao pamoja na wawekazaji wadogo wa umeme wa umeme nchini kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati,Mkoani Dodoma
Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga(kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Dkt Tito Mwinuka(katikati) wakiwa kwenye kikao pamoja na wawekazaji wadogo wa umeme wa umeme nchini kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati,Mkoani Dodoma
Picha mbalimbali za Washiriki wa kikao kati ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake pamoja na Wawekezaji wadogo wa Umeme wa nchini wakiwa kwenye kikao pamoja na wawekazaji wadogo wa umeme wa umeme nchini kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati,Mkoani Dodoma
………………………………………………………………………………..
Hafsa Omar-Dodoma
Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani,amewataka wazalishaji Wadogo wa Umeme nchini kuzingatia maelekezo ya Serikali ya kupunguza bei ya umeme katika maeneo ambayo wanatoa hudumua hiyo.
Ameyasema hayo Agosti 6,2020, wakati alipokuwa na kikao na wazalishaji Wadogo wa Umeme Nchini,kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati,Mkoani Dodoma.
Katika kikao hicho, aliambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu Mhandisi Zena Said, Naibu Katibu Mkuu Mhandishi Leornad Masanja, na viongozi mbalimbali wa Wizara na Taasisi zake.
Aidha, amewaeleza wawekezaji hao kuwa Serikali haitatoa mda wa ziada wa majadiliano kuhusu jambo hilo, kwasababu Serikali imeshatoa mda wa kutosha wa kuwasikiliza wawekezaji hao na kwasasa kilichobaki ni utekelezaji wa maagizo hayo.
“Tumekaa hapa pamoja ili kuona namna bora kwenda kulitatua jambo hili, takribani miaka 10 iliyopita tulifungua milango kwa uwekezaji kuja kuwekeza na tunaendelea kufungua milango hiyo lakini tunataka uwekezaji yenye manufaa kwa pande zote mbili nyinyi mpate faida na wananchi pia wapate huduma yenye manufaa kwao,”alisema.
Aliongeza kuwa, ni matarajio ya Watanzania kuona manufaa ya kazi za wawekazaji hao,na Serikali itahakikisha inasimamia na kuondoa kero zote ambazo zimejitokeza katika miradi hiyo.
Alieleza kuwa, bei ya kuunganisha umeme kwa wateja kwa maeneo ambayo wawekezaji hao wanatekeleza miradi hiyo hailingani na uhalisia wa hali ya maisha wananchi wa kawaida wa maeneo hayo ambapo wananchi wengi wanashindwa kulipia huduma hiyo kutokana na gharama kubwa wanazotozwa.
Aliongeza kuwa,bili ya umeme kwa wateja nchini lazima iwe moja kwasababu nchi ni moja na bei lazima zilingane na haiwezekani nchi moja kuwe na bei tofauti za huduma hiyo ya umeme na Serikali haipo tayari kuona hayo.
Alifafanua kuwa, Serikali imefanya ukaguzi na kugundua kuwa kuna kero nyingi sana ambazo wananchi wanazipata za jinsi ambavyo wawekezaji hao wanavyowahudumia wateja wao, ambapo wananchi wengi wameeleza kero ya kupata umeme mdogo ambao hauwatoshelezi kwenye kujikwamua kiuchumi,
“ kuna kero nyingi lakini kero kubwa ni namna ya uunganishaji wa umeme wananchi wengi wamelalamika umeme ni mdogo hauna nguvu hiyo ni kero lazima tuikubali tunajenga uchumi wa Viwanda huwezi kumpelekea umeme mwananchi wa kuwasha taa peke yake tu lazima umeme umsaidie mwananchi kwa shughuli za kiuchumi,”alisema.
Dkt Kalemani, amewashukuru wakezaji hao kwa ushirikiano wao na kuona umuhimu wa kushughulikia jambo hilo ambalo ninawatesa wananchi wengi,kwasababu wateja wengi wa maeneo hayo ni wa hali ya chini na wanategemea nishati ya umeme wa gharama nafuu kuishi na kufanya shughuli zao za kiuchumi .
Kwa upande wake, Mhandisi Matthew Matimbwi ambae ni mzalishaji wa umeme amesema wamepokea kauli hiyo kwa mikono miwili na wapo tayari kushirikiana na Serikali kutatua kero hizo ambazo zinawapata watanzania wanaishi maeneo ya pembezoni.
Amesema kuwa, kwa upande wao wapo tayari kuendelea na kazi ya kuzalisha umeme ili wananchi ambao wanaishi pembezoni waendelee kupata nishati ya umeme jadidifu na wapate umeme huo kwa bei ambayo Serikali imependekeza.