Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu, barua pepe, ujumbe mfupi na mitandao ya kijamii leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akiangalia namna kituo cha huduma kwa wateja kinavyofanya kazi baada ya uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu, barua pepe, ujumbe mfupi na mitandao ya kijamii leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akipata maelekezo kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa wateja TAMISEMI, Bi. Antelma Mtemahanji pale mteja anapopiga simu .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza na watendaji wanao hudumu katika kituo cha huduma kwa wateja TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wanao hudumu katika kituo cha huduma kwa wateja TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Wakurungenzi wa Idara za TAMISEMI .
………………………………………………………..
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema kuwa wameanzisha kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu, barua pepe, ujumbe mfupi na mitandao ya kijamii ili kuboresha huduma zake katika kuwahudumia watanzania kwa haraka na ufasaha.
Mhe. Jafo amebainisha hayo leo Jijini Dodoma katika uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa wateja Ofisi ya Rais TAMISEMI uliyofanyika katika ofisi zao.
Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa lengo kuu la kuanzisha kituo hicho ni kumuundolea mteja usumbufu usio kuwa wa lazima ili abaki katika maeneo ya makazi yake akiendelea na utafutaji wake ili kuleta maendeleo katika nchi.
“Kwa sasa wananchi hawatakuwa wakisafiri mwendo mrefu na kuingia gharama zisizo za lazima , wakina mama walikuwa wakisafiri na watoto mgongoni kufata huduma hapa hivyo tumieni vyema nafasi hii kueleza kero ili kuweza kuhudumiwa bila usumbufu wowote.
Mhe. Jafo akizindua kituo hicho amepata kutaja namba ya kupiga bure ili kuhudumiwa kuwa ni +255 262 160 210 na kumpokea mmoja wa wateja aliyepiga simu akiuliza utaratibu wa wanafunzi wa chaguo la pili waliomaliza kidato cha Nne wanachaguliwa lini?
“Ndugu mteja wanafunzi wa chaguo la pili bado wanapangiwa shle hivyo naomba uwe na subira kwani ndani ya muda mfupi tutatangaza wanafunzi waliochaguliwa awamu ya pili, mwanao anaufaulu gani? asante na karibu tena tukuhudumie”, amezngumza Mhe.Jafo wakati akimsiliz mteja.
Kwa kuongezea Mhe.Jafo amesema kuna ulazima wa kuanzisha Television ya TAMISEMI itakayokuwa inaeleza utendaji wa serikali wakati kwa wananchi wake.
Katika hatua nyingine Mhe. Jafo amesema kuwa kunahaja ya kuhacha alama katika utendaji wa watumishi wa TAMISEMI ili kuleta faida kubwa kwa vizazi vijavyo kuwa na weledi wa kuwajibika kwa taifa lao.
Mhe. Jafo ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa hiyo kuhudumiwa ili kutatuliwa matatizo yao kwa wakati na kuendelea na shughuli zao bila kuwa na vikwazo kuhusu huduma zinazotolewa na serikali yao.
Naye Katibu Mkuu TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga ameeleza kuwa watanzania wasirubuniwe na watu wasio wazuri kwa serikali yao kwa kuwatoza hela kuwa watawasaidia katika kuwahudumia hasa katika swala la huamisho.
“Kabla ya kuwa na mfumo huu watuwengi wamekuwa wakitapeliwa na wengine kutoa rushwa ili ksaidiwa katika mambo ya huamisho na baadhi wamekamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na wengine tunaendelea na msako”, ameweka wazi Nyamhanga.
Awali Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa wateja TAMISEMI, Bi. Antelma Mtemahanji ameeleza namna mfumo huo utaweza kufanya kazi na kusema kuwa unasaidia pia kuonyesha utendaji kazi wa watmishi wanaofanya kazi katika kituo hicho.
Mtemahanji amesema kuwa kauli mbiu ya kituo hicho katika utoaji huduma kwa wananchi ni “Mabadiliko ni Mimi na Wewe Kituo cha Huduma kwa Wateja TAMISEMI Tunawajibika”.