Home Burudani WADAU SEKTA YA UTALII WAZOA TUZO ZA TANAPA ZA UTALII MWAKA JIJINI...

WADAU SEKTA YA UTALII WAZOA TUZO ZA TANAPA ZA UTALII MWAKA JIJINI ARUSHA

0

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa tuzo za TANAPA 2020 kwa watoa huduma  za utalii Bora kwa mwaka 2020 jijini Arusha leo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa Tuzo ya utoaji huduma za Utalii ya TANAPA 2020 kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ahsante Tours, Cuthbert Swai leo jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa Tuzo ya utoaji huduma Bora za Utalii ya TANAPA 2020 kwa Mmiliki na Mwanzilishi wa Kampuni ya Zara Tours, Zainab Ansell leo jijini Arusha. Wengine wanaoshuhudia Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo huku akiwa ameshika moja ya Tuzo alizokua  akitoa kwa watoa huduma bora za utalii wa sekta binafsi leo jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza na wadau wa sekta ya Utalii wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Utalii za TANAPA kwa mwaka 2020 leo jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara akizungumza na wadau wa sekta ya Utalii wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo za Utalii za TANAPA kwa mwaka 2020 leo jijini Arusha.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Kamishina Mkuu wa Uhifadhi wa TANAPA Dkt. Allan Kijazi akizungumza na wadau wa sekta ya Utalii leo jijini Arusha wakati wa hafla fupi ya utoaji wa Tuzo za Utalii za TANAPA 2020 jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya  Tuzo za TANAPA 2020 alizokua akitoa kwa wadau wa sekta ya Utalii leo jijini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki akielezea faida ya Tuzo za TANAPA za utalii kwa wadau waliohudhuria tuzo za TANAPA za Utalii kwa Mwaka 2020, zilizofanyika mapema leo Jijini Arusha..

Waziri wa Maliasi na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (wapili kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce K. Nzuki (kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Waitara (wapili kulia) wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Utalii za  TANAPA Jijini Arusha.

 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa tuzo za utalii za TANAPA 2020 kwa mwakilishi wa kampuni ya Leopard Tour E. Kimario jijini Arusha leo.

PICHA/Aron Msigwa – WMU.