Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Gabriel Malata (kulia) akimkabidhi taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwingulu Nchemba leo jijini Dar es Salaam.
Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Gabriel Malata (kulia) akimkabidhi taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju (kushoto) leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwingulu Nchemba akifafanua jambo wakati akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es Salaam.
Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Gabriel Malata (kushoto) akiteta jambo na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende wakati wakiwa katika kikao kazi na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwingulu Nchemba leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Tanzania wakiwa katika kikao kazi na Waziri Dkt. Mwingulu Nchemba leo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea ofisi hiyo.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwingulu Nchemba akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
*************************************
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwingulu Nchemba amewataka watendaji wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa vitendo ikiwemo kusimamia mashauri mbalimbali kwa uweledi ili kuhakikisha haki inapatikana kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Nchemba, amesema kuwa hatapenda kuona uzembe unafanywa kwa mawakili wasomi wa serikali katika kusimamia haki.
‘Mtendaji yoyote akifanya kosa ambalo litaleta madhara kwa taifa kupitia utendaji wake, atachukuliwa hatua za kisheria kuwa amehujumu uchumi” amesema Dkt. Nchemba.
Amesema kuwa ni vizuri mawakili kuacha kufanya kazi kwa mazoea, badala yake kuendelea kulinda rasilimali za taifa kwa wivu mkubwa ili kuokoa mali za watanzania katika kutafuta haki.
Amefafanua kuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanzisha taasisi hiyo ili kuongeza ufanisi katika vita ya uchumi na sio kuongeza nafasi za ajira.
“Sitapenda kusikia jambo kubwa lenye maslahi mapana ya taifa linashindwa kufanikiwa katika kuhakikisha haki inapatikana….baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kuiba na kwenda kujificha katika kichaka cha sheria’ amesema Dkt. Nchemba.
Hata hivyo ameeleza kuwa anaamini watendaji wote wa ofisi ya wakili mkuu wa serikali wataendelea kufanya kazi kwa uweledi ikiwemo kutowaficha wahalifu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju, amesema kuwa ofisi ya wakili Mkuu wa serikali ina umuhimu mkubwa katika kuhakikisha taifa linasonga mbele kimaendeleo.
Bw. Mpanju ameeleza kuwa baada ya matokeo kuchaguzi mkuu, baadhi ya wagomea wamekuwa na tabia ya kupinga matokeo mahakamani kwa kuweka pingamiza, hivyo anatarajia kuona mawakili wasomi wanaendelea kutetea haki ya ajili ya mslahi mapana ya taifa.
Kwa upande wake, Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Gabriel Malata, amesema kuwa ofisi yake imekuwa ikiendesha mashauri mbalimbali ndani na nje ambayo yamefunguliwa katika mahakama za Afrika Mashariki na nchi mbalimbali duniani.
Amesema kuwa pia wamekuwa wakitoa maelekezo ya mambo yote ya kisheria kwa kutoa ushauri mzuri wa madai ya suluhisho katika mashirika na taasisi zote za serikali.
Ameelema kuwa wamekuwa wanahakikisha wanapata idadi ya mashauri yote madai yanayohusu serikali na mashirika, na mashauri ili kutambua mashauri yasiokuwa na tija pamoja na yenye maskahi mapana kwa taifa.
Wakili Malata amesema Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali itaendelea kufanya kazi kwa uweledi ili kuhakikisha taifa linasonga mbele kimaendeleo.