Home Mchanganyiko EWURA BEI MPYA ZA MAFUTA KUANZA KUTUMIKA KESHO

EWURA BEI MPYA ZA MAFUTA KUANZA KUTUMIKA KESHO

0

Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo wakati akitoa taarifa ya hali ya mafuta nchini.

Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia taarifa ya hali ya mafuta iliyokua ikitolewa na Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo leo jijini Dodoma.

 …………………………………………….

Na. Majid Abdulkarim ,Dodoma

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji Nchini (EWURA) imesema kuwa bei mpya za mafuta zitaanza kutumika kesho Agast 5 katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa  EWURA, Titus Kaguo  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma.

Kaguo amesema kuwa Dar es Salaam, Petroli imepanda kutoka Sh. 1693 hadi Sh. 1832, Tanga kutoka Sh. 1654 hadi 1868, Mtwara kutoka Sh.1612 hadi 1875 huku kwa upande wa Dizeli kwa Tanga ikipanda kutoka Sh. 1693 hadi 1778 na Mtwara kutoka Sh. 1731 hadi 1799.

Aidha Kaguo amesema licha ya kupanda kwa bei hizo  za mafuta kati ya Meli sita za petroli zilizotarajiwa kuingia nchini kuanzia Julai 29 hadi Agosti 31 mwaka huu, tayari Meli tatu zimewasili nchini zikiwa na jumla ya lita milioni 89.564 kwa ajili ya soko la ndani .

“Kiasi hicho kitatosheleza mahitaji ya nchi kwa zaidi ya siku 18 huku Meli tatu nyingine zikitarajiwa kuwasili kati ya Agosti 17 na Agosti 31 mwaka huu zikiwa na lita takribani milioni 100.075 zitakazotosheleza mahitaji ya nchi kwa zaidi ya siku 22” ameeleza Kaguo.

Kaguo amesisitiza kuwa mafuta ya dizeli yapo ya kutosa na Meli tatu za mafuta hayo zenye jumla ya lita milioni 193.391 zinategemewa kuingia nchini Agosti mwaka huu hivyo wanawakika wa kimiri mahitaji ya nchi.

Kwa kuongezea Kaguo amesema kuanzia Juni 2020 matumizi ya petroli yaliongezeka kufikia lita mil.3.683 kwa siku na Julai 2020 matumizi yaliongezeka  zaidi kufikia lita mil.4.425 kwa siku ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 21.

Katika hatua nyingine Kaguo amebainisha kuwa pamoja na ongezeko hilo akiba ya mafuta iliyokuwepo katika magahala iliendelea kutosheleza mahitaji ya nchi

“Ili kuwa na utoshelevu wa mafuta nchini,kuanzia Septemba 2020 EWURA imeongeza makadirio ya matumizi ya mafuta kwa siku kuwa lita mil.4.812 kwa petrol na lita mil.6.082 kwa dizeli”,amesema Kaguo.

 Kaguo amesema mamlaka wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA) atatumia makadirio haya wakati wa kuagiza mafuta ili kuweza kuwa na uimara zaidi juu ya nishati ya mafuta kwa watumiaji nchini.

Hata hivyo a Kaguo amesema kuwa Kanda  ya Ziwa inayohusisha mikoa ya Mwanza,Mara,Simiyu,Kagera na Kigoma mafuta yanapatikana isipokuwa kuna uhaba umejitokeza katika Wilaya za Bunda na Musoma mkoani Mara.

“Hii inatokana na kuchelewa kuondoka kwa magari ya mafuta kutoka Dar es salaam kuelekea maeneo hayo hasa kwa kuzingatia kuwa kulikuwa na siku tatu ambazo siyo za kazitangui ijumaa ya julai 31 mwaka huu”, amebainisha Kaguo.

Naye Meneja Biashara wa EWURA, Kemilembe Kafanabo ameeleza  sababu za bei kuwa tofauti katika Mikoa ya Tanga na Mtwara, ni kutokana na bei kutofautiana katika soko la dunia.