Home Michezo ARSENAL YATWAA KOMBE LA FA BAADA YA KUTOKA NYUMA NA KUICHAPA 2-1...

ARSENAL YATWAA KOMBE LA FA BAADA YA KUTOKA NYUMA NA KUICHAPA 2-1 CHELSEA

0

Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang akiwa ameinua Kombe la FA baada ya kuiongoza Arsenal kubeba hilo kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea Uwanja wa Wembley Jijini London usiku wa leo. Chelsea walitangulia kwa bao Christian Pulisic dakika ya tano kabla ya Aubameyang kusawazisha kwa penalti dakika ya 28 na kufunga la ushindi dakika ya 67 kuipa The Gunners taji la 14 la FA akiwa amevaa jezi namba 14 mgongoni. Chelsea ilimaliza pungufu baada ya Mateo Kovacic kutolewa kwa kadi nyekundu na refa Anthony Taylor kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 72 PICHA ZAIDI SOMA HAPA