Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ndugu. Aron Kagurumjuli wakikagua bidhaa za wajasiriamali wanaosindika chakula katika Banda la maonesho ya wakulima Nanenane mkoani Morogoro. Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Patricia Henjewele akimuelezea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Profesa Mbaramagamba Kabudi kuhusu kilimo cha kisasa Cha mjini na Vijijini. Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifaa, Profesa Paramagamba Kabudi akikagua bidhaa za wajasiriamali wa usindikikaji chakula kutoka Manispaa ya Kinondoni leo alipotembelea Banda hilo. Mwenyetisheti jekundu ni Mkuu wa Idara na Ushirika Salehe Hija, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo.Muonekano wa Banda la maonesho ya Wakulima Nanenane la Manispaa ya Kinondoni lililopo mkoani Morogoro.
*************************************
Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Profesa Paramagamba Kabudi ametembelea Banda la Kinondoni katika maonesho ya wakulima ya nanenane Mkoani Morogoro nakuipongeza kwakuwa na vitu ambavyo vinavutia watazamaji.
Profesa Kabudi amesema katika Banda hilo amevutiwa na Teknolojia ya kilimo Cha mjini na Vijijini ikiwemo kilimo Cha kisasa cha mbogamboga na mazao ya chakula sambamba na ufugaji wa kisasa.
Ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo wananchi wa Dar es Salaam wanakila sababu ya kujifunza teknolojia hizo kutoka Manispaa ya Kinondoni kwakuwa itawawezesha kuendesha shuguli zao za kilimo Cha mijini.
Amesema katika Banda hilo pia amevutiwa na wajasiriamli wakina Mama wanaotengeneza bidhaa za nguo kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ambao inaongeza thamani ya bidhaa hiyo na hivyo kumpongeza Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kuwawezesha wajasiriamali hao.
” Mkurugenzi nakupongeza wewe pamoja na timu nzima ya Kinondoni, mmefanya kazi kubwa kwenye maonesho hayo, mmewaletea Wananchi mambo mazuri ambapo wanapokuja kuangalia wanaondoka na ujuzi mzuri katika nyanja zote ikiwemo kilimo, ufugaji, usindikikaji wa vyakula na utengenezaji wa bidhaa za nguo za batiki.
Aidha ameipongeza Manispaa hiyo kwa kuwawezesha vijana wajasiriamali katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi ikiwemo viatu nakusema kuwa mpango huo ni mzuri kwani unaendana sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya Viwanda ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Ameongeza kuwa Rais Magufuli anaguswa na vijana ambao wanatumia ujuzi wao kwa ajili ya kuijenga nchi na kwamba Manispaa imeonambali katika kuwawezesha kwenye ufanisi huo ambao unatija kwa Taifa.